“Njoni Kwangu,” Kwa Ajili ya Nguvu Kwa Vijana, Machi 2023.
Mstari juu ya Mstari
Njoni Kwake
Mwokozi anatualika sisi kumwachia Yeye abebe mizigo yetu.
Njoni Kwangu
Tunaweza kuja kwa Mwokozi kwa kujifunza injili Yake, tukiwa na imani katika Yeye, tukitubu, tukifanya na kushika maagano na kufuata mfano Wake.
msumbukao … kulemewa na mzigo
Kazi za kimwili na mizigo vinaweza kutulemea, kadhalika na za kiakili, kihisia na kiroho. Mwokozi hutupa sisi amani Yake, bila kujali aina ya mizigo tunayobeba.
nira
Nira ni kifaa cha kufunga wanyama wawili pamoja ili kwamba waweze kuvuta mzigo kwa pamoja, kama vile jembe la plau au mkokoteni. Nira kwa kawaida ina boriti ya mbao inayowekwa juu ya nundu ya mabega ya kila mnyama, kufanya uzito kuwa sawa.
jifunze
Tunaweza kujua kuhusu Yesu Kristo kwa kujifunza mafundisho Yake na mfano Wake—na kwa kujaribu kuyafuata
pumziko
Pumziko la Mwokozi ni amani Yake, ambayo hutuliza akili na roho zetu. Yeye hutusaidia kushinda wasiwasi wa ulimwengu na hutupa nguvu za kiroho wakati tunapohisi udhaifu.
laini … mwepesi
Kujichukulia juu yetu nira ya Mwokozi humaanisha kujifunga wenyewe Kwake kupitia maagano. Humaanisha kutoa mioyo yetu Kwake na kazi Yake. Tunapofanya hivi, mizigo yetu inasikika kuwa miepesi kwa sababu Yeye anatusaidia.