2023
Kanuni Kuu, Chaguzi Maalumu
Machi 2023


“Kanuni Kuu, Chaguzi Maalumu ,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Machi 2023.

Kanuni Kuu, Chaguzi Maalumu

Ni kwa jinsi gani wewe unatumia kanuni kuu katika hali maalumu katika maisha yako?

msichana katika kioo cha kukuza

Kielelezo na Josh Talbot

Hapa kuna nukuu tatu kutoka kwa manabii watatu tofauti. Ona kama unaweza kugundua dhima sawa:

“Ee pokeeni hekima; niseme nini zaidi?”

“Siwezi kuwaelezea vitu vyote ambavyo vinaweza kuwasababisha kutenda dhambi.”

“Ninawafundisha kanuni sahihi, na wanajiongoza wenyewe.”

Teachings of Presidents of the Church: Joseph Smith (2007), 284.

Inaonekana kwamba manabii hutupa sisi kanuni za injili ya Bwana, na kisha wanatuachia sisi tuziishi. Wao hawatupatii sisi maelezo yote. Kwa hiyo, ni kwa jinsi gani tutachukua mafundisho yao na kuyatumia?

Ni kwa Jinsi Gani Unayatumia Mafundisho ya Manabii?

Manabii hutupatia sisi amri kutoka kwa Bwana. Wanatufundisha sisi kanuni na miongozo ambayo inatusaidia sisi kutumia kweli na amri za milele—kwa mfano, katika mwongozo wa Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana.

Lakini waumini wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho wakati mwingine wanajiuliza kuhusu maelezo ya kina—mambo maalumu tunayopaswa kufanya ili kuishi vyema kanuni na amri za injili. Kwa mfano, watu wanaweza kujiuliza hasa ni aina gani ya mavazi huonyesha heshima stahiki kwa miili yao. Au wanaweza kujiuliza ni nini hasa wanapaswa kufanya siku ya Sabato ili kuitakasa.

Kanuni kuu zinaweza kutumika katika njia maalumu tofauti na watu tofauti, lakini tunaweza kutafuta maelekezo ya Bwana tunapofanya chaguzi zetu binafsi ili kwamba tuweze kusogea karibu zaidi na Mungu.

Mpangilio wenye Msaada

Rais Russell M. Nelson wakati mmoja alielezea jinsi yeye hufanya chaguzi kuhusu kuitakasa siku ya Sabato:

“Nilijifunza kutoka kwenye maandiko kwamba tabia yangu na mtazamo wangu juu ya Sabato vinafanya ishara iliyoko kati yangu mimi na Baba yangu wa Mbinguni. Kwa uelewa huo, sikuhitaji tena orodha ya vya kufanya na vya kutofanya. Nilipohitaji kufanya maamuzi ya kujua kama shughuli ilikuwa au haikuwa sahihi kwa ajili ya Sabato, nilijiuliza mwenyewe tu, ‘Ni ishara gani ninataka kumwonyesha Mungu?’ Swali hilo lilifanya uchaguzi wangu kuhusu siku ya Sabato kuwa muhimu zaidi” (mkutano mkuu wa Apr. 2015 [Ensign au Liahona, Mei 2015, 130]).

Njia ambayo Rais Nelson alitazama swali hili muhimu inaweza kutuonyesha sisi mpangilio mkuu wa kufanya chaguzi kuhusu amri na miongozo. Hapa kuna njia moja ya kuionyesha:

Unaweza kufuata mpangilio huu kwa kila amri au mwongozo—Neno la Hekima, vyombo vya habari na burudani, muziki, usafi wa kimwili na hata zaka. Itahitaji bidii, lakini ina thamani.

Unapojifunza mambo haya, unaweza kusoma kile maandiko na manabii wanachosema juu yake, tafakari na usali kwa Baba wa Mbinguni. Kisha Roho Mtakatifu anaweza kukusaidia na kukuongoza kufanya chaguzi nzuri.

Je, vipi kuhusu Chaguzi za Wengine?

Tambua kwamba Rais Nelson hakutuambia sisi chaguzi muhimu ambazo alifanya kuhusu siku ya Sabato. Alituonyesha jinsi ambavyo tunaweza kufanya chaguzi zetu wenyewe. Unaweza kufanya nyingi za chaguzi zile zile alizofanya. Lakini jambo muhimu ni kujaribu kusogea karibu zaidi na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo kupitia chaguzi zetu.

Kama ukigundua mtu mwingine katika Kanisa ambaye hafanyi kila kitu hasa kama vile unavyofanya wewe, hauna haja ya kuwa na wasiwasi kuhusu kuwasahihisha. Kama Reyna I. Aburto, Mshauri wa Plil mstaafu katika Urais wa Muungano wa Usaidizi wa Akina Mama wakati mmoja alisema , “Acha tufuate njia ya Mwokozi na kuzidisha huruma yetu, kupunguza tabia yetu ya kuhukumu na kuacha kuwa wakaguzi wa hali ya kiroho ya wengine.” (mkutano mkuu wa Okt. 2019 [Ensign au Liahona, Nov. 2019, 58]).

Unaweza kukumbatia kanuni sahihi zinazofundishwa na manabii. Unaweza kuwaelekeza wengine kwa Mwokozi, upendo Wake, huruma Yake na amri Zake. Unaweza kusoma mwongozo wa Kwa Ajili ya Nguvu Kwa Vijana. Unaweza kujaribu kuishi maisha ya uaminifu kama mwanafunzi wa Yesu Kristo, uwe mfano mzuri na kushiriki uzoefu wako wa kiroho.

Ukifokasi kwenye kumpenda Mungu na kuwapenda wengine, utaongozwa kufanya chaguzi ambazo zitakusaidia kukufanya wewe na wengine kuwa na furaha.