“Jinsi Mwokozi Aliwatendea Wanawake,” Kwa Ajili ya Nguvu Kwa Vijana, Machi 2023.
Jinsi Mwokozi Aliwatendea Wanawake
Tunaweza kufuata mfano wa Yesu Kristo wa kuonyesha ukarimu na heshima kwa wanawake katika maisha yetu.
Katika Agano Jipya, Yesu Kristo kila mara anafundisha vitu visivyotarajiwa. (Kama vile: Tunapaswa kuwapenda maadui zetu na kuwaombea wale wanaotutesa?1
Baadhi ya mafundisho haya yalikiuka tamaduni za wakati huo. Lakini Mwokozi hakuwa akijaribu kukubalika. Yeye alikuwa anajaribu kufundisha sheria ya juu na kutuonyesha jinsi ya kutendeana. Yeye alikuwa anaweka mfano wa upendo ambao haukuwa na kikomo cha umri fulani, jinsia au utaifa.
Katika wakati wa Yesu, wanawake walikuwa kwa kawaida wanatendewa kama watu duni. Na katika baadhi ya tamaduni leo, wanawake kwa kawaida hawatendewi kwa heshima. Labda wewe unaishi katika sehemu kama hizo. Ikiwa ndivyo, wewe unaweza kuweka mfano kama wa Kristo kwenye jumuiya yako kwa kuwa mpole na mwenye heshima kwa kila mtu—ikijumuisha wasichana na wanawake katika maisha yako.
Yesu Alimjali Mama Yake
Muujiza wa kwanza wa Yesu Kristo mbele ya umati wa watu ulikuwa mmoja wa kumsaidia mama Yake. Mama alikuwa na jukumu la kusaidia kuwalisha watu katika harusi. Wakati walipoishiwa na vinywaji, Yesu aligeuza maji kuwa mvinyo ili kuwe na mvinyo ya kutosha kwa ajili ya wageni.
Maneno ya majibu ya Yesu kwa mama Yake katika mazungumzo hayo yaweza kuonekana kama makali kwa masikio yetu ya kisasa: “Mama, tuna nini mimi nawe?” (Yohana 2:4). Lakini Joseph Smith alifafanua kwamba Yesu alikuwa anamuuliza mama Yake, “Mwanamke, ni kitu gani ungetaka mimi nikifanye kwa ajili yako?”2. Na kumwita mtu “mwanamke” zama hizo ilikuwa neno la heshima. Yeye kimsingi alikuwa anasema, “Mwanamke wangu, chochote utakachoniomba kwa imani, nitakupa.”3
Kusonga mbele karibia miaka mitatu tu. Kabla tu ya Yeye kufa msalabani, mojawapo ya mambo ya mwisho Yesu aliyofanya ilikuwa ni kuhakikisha mama Yake anatunzwa.
“Yeye alimwambia mama yake, Mwanamke, tazama mwanao! “Kisha akamwambia yule mwanafunzi, Tazama, mama yako! Na tangu saa ile mwanafunzi yule akamchukua nyumbani kwake” (Yohana 19:26–27).
Yesu Aliwatendea Wanawake Waliotengwa kwa Heshima
Tunayo angalau mifano miwili ya Mwokozi akiwatendea wanawake kwa heshima ambao walikuwa wametengwa na jamii.
Katika wakati wa Mwokozi, wengi wa Wayahudi waliwadharau watu Wasamaria. Lakini Yesu Kristo alipokutana na mwanamke Msamaria kisimani, Yeye alimtendea kwa huruma na heshima. Zaidi ya hayo, ilikuwa wakati akizungumza na yule mwanamke ambapo Yesu alijifunua Yeye Mwenyewe kwamba alikuwa ndiye Mwokozi mwahidiwa!4 (Ona Yohana 4.)
Katika hali nyingine, mwanamke alifumaniwa katika dhambi kubwa. Kulingana na sheria ya Wayahudi, yeye angepigwa kwa mawe hadi kifo. Wakati viongozi walipomleta mwanamke huyu mbele ya Mwokozi, Yeye aliwauliza wao swali ambalo lilisababisha wao kusita na kufikiria. Hawakumpiga kwa mawe. Kisha Mwokozi alimwalika kutubu, akisema, “Enenda zako; wala usitende dhambi tena” (Yohana 8:11).
Yesu Aliwatokea Wanawake baada ya Kufufuka Kwake
Baada ya Yesu kufufuka, Yeye kwanza alimtembelea Mariamu Magdalena, ambaye alikuwa anaomboleza kwenye kaburi Lake (ona Yohana 20:11–18). Wanawake wengine—Yoana, vile vile Mariamu mama yake Yakobo—walikuwa miongoni mwa watu wa kwanza kujua kuhusu Bwana aliyefufuka. Malaika aliwaalika kushiriki shuhuda zao juu ya kile walichokuwa wameona. (Ona Luka 24:1–10.)
Tunaweza Kufuata Mfano Wake
Tunaweza kufanya nini ili kufuata mfano wa Mwokozi wa kuwaheshimu wanawake?
Nabii wetu, Rais Russell M. Nelson, ana uzoefu mwingi katika eneo hili. Yeye amewalea mabinti tisa na mwana mmoja pamoja na mke wake Dantzel. Baada ya Dantzel kufariki, amemuoa Wendy Nelson.
“Sisi tunawaheshimu wakina dada—sio tu wale wanaotoka katika familia zetu wenyewe bali wakina dada wote wazuri katika maisha yetu,” yeye alifundisha.5
Acha tuufanye mwezi huu kuwa mwezi wa ujasiri, upendo kama Kristo na ukarimu kwa wanawake walio katika maisha yetu. Ninyi mnazo nguvu nyingi za kutosha kubadilisha ulimwengu huu, uhusiano mmoja kwa wakati mmoja!