Wakati Hekalu la Salt Lake lilikamilishwa mwaka 1893, Watakatifu wa Siku za Mwisho walifurahia. Ilikuwa imechukua miaka 40 ya kulijenga hekalu. Kwa sababu watoto walikuwa wamechanga fedha kusaidia kujenga hekalu, Rais Wilford Woodruff aliamua kufanya vikao vitano vya kuweka wakfu maalum kwa ajili ya watoto kuhudhuria.
Leo mahekalu ni mengi duniani, na watoto bado husherehekea kukamilika kwa mahekalu. Angalia jinsi watoto wameshiriki siku hizo na sasa.
Zaidi ya watoto 12,000 walikuja katika Hekalu la Salt Lake kwa uwekaji wakfu. Watoto hawa kutoka Kata ya Sugar House walipanda gari moshi.
Tikiti hii iliwaruhusu watoto wa umri hadi miaka 16 kuhudhuria mikutano maalum ya kuweka wakfu kwa ajili ya Hekalu la Salt Lake. Mitume na washiriki wa Urais wa Kwanza walihotubia watoto waliokuwa ndani ya hekalu.
Wakati mwingine mahekalu huwekwa wakfu upya baada ya kutengezwa upya. Watoto wa msingi waliimba na kubeba mataa katika utendaji uliosherehekea kuwekwa wakfu upya kwa Hekalu la Anchorage Alaska.
Kila wiki kama Hekalu la Gilbert Arizona linajengwa, watoto wa Msingi kutoka Kigingi cha Gilbert Arizona Highland wameweka lengo kumtumikia mtu fulani katika kata zao.
Wakati Hekalu la San Diego California lilijengwa, watoto wa Msingi kutoka Mexico walitengeneza zulia la rangi nyingi kwa hekalu. Viongozi Wenye Mamlaka walisimama juu ya zulia wakati wa huduma ya jiwe la tao la pembeni katika kuwekwa wakfu.
Watoto wa Msingi kutoka Manitoba, Kanada, walisafiri kwa gari masaa matatu kuenda Hekalu la Regina Saskatchewan kugusa kuta na kujitolea kwenda ndani siku moja.
Watoto wa Msingi katika ufunguzi wa Hekalu la Kyiv Ukraine waliwakaribisha wageni kwa kuimba “Napendelea Kuona Hekalu”.
Zaidi ya 800 Watoto wa Msingi kutoka Afrika Magharibi waliimba “Mimi ni Mtoto wa Mungu” katika sherehe za kitamaduni kabla ya kuwekwa wakfu kwa Hekalu la Accra Ghana.
Kila hekalu lina jiwe la tao la msingi linaloonyesha mwaka liliwekwa wakfu. Wakati wa kuwekwa wakfu, Wenye Mamlaka Mkuu hufunga jiwe la tao la pembeni kwa simiti. Isaac B., umri miaka 9, alisaidia kuweka simiti juu ya jiwe la tao la pembeni la Hekalu la Kansas City Missouri.
Watoto wa msingi walimwimbia Rais Gordon B. Hinckley alipofika kuweka wakfu Hekalu la Aba Nigeria.