2013
Kuvutiwa Hekaluni
Aprili 2013


Kuvutiwa Hekaluni

Mzee Jairo Mazzagardi

Kwa wengi wa watu wema, hekalu huvutia hisia ambazo zinaweza kwa mara moja kuingia moyoni.

Kabla niitwe kama mshiriki wa Jamii ya Pili ya Wale Sabini, mke wangu nami tulikaa miaka mingi tukihudumu katika Mahekalu ya Campinas na São Paulo Brazil. Katika mahekalu yote mawili, nilishangazwa mara nyingi kuwa watu waliosafari kupita karibu na hekalu wangevutiwa kwake hadi wangesimama, waingie na kuuliza juu yake.

Walipoingia, tuliwajulisha kuwa hawangeweza kuendelea mbele zaidi bila matayarisho yafaayo. Kisha tulielezea lengo la hekalu, tukashiriki mafundisho machache ya msingi ya injili, na kuwaalika wao kukutana na wamisionari. Kwa wengi wa watu wema, hekalu lenyewe ni mmisionari mkuu kwa sababu linavutia hisia zinazoweza kwa mara moja kuingia moyoni.

Mke wangu, Elizabeth, nami tunazijua nguvu za hisia kama hivyo kihasili. Karibu miaka 40 iliyopita, rafiki mzuri na mwenzangu, mshiriki wa Kanisa, alianza kuleta mambo ya injili kwetu katika mazungumzo ya kawaida. Kwa mara kadha, aliwatuma wamisionari kututembelea. Tuliwapenda wamisionari na tukakubali kuchukua mafunzo, lakini hatukuwa na moyo wa kupendelea kujua yale waliyokuwa nayo ya kufundisha.

Hayo yalibadilika mnamo Oktoba 1978, ambapo mwenzangu aliwaalika marafiki kadhaa, ikitujumuisha sisi, katika ufunguzi wa Hekalu la São Paulo Brazil. Alikomboa mabasi kadhaa yeye mwenyewe ili marafiki zake wangeambatana naye hekaluni, umbali wa karibu maili 50 (80km).

Wakati Elizabeth alipoingia mahali pa kubatiza, alihisi kitu ambacho kamwe hajawaihisi tena, kitu ambacho aligundua baadaye kuwa Roho Mtakatifu. Hisia hio ilikuwa ni furaha tele moyoni mwake. Alijua katika dakika hio kuwa Kanisa lilikuwa la kweli na kuwa lilikuwa Kanisa alilotaka kushiriki.

Hisia sawa na hio ilinijia mimi mwishoni mwa ufunguzi huo, tulipotembezwa katika chumba cha kuunganisha na kufundishwa fundisho la familia za milele. Fundisho hilo lilinigusa mimi. Nilikuwa nimefuzu katika weledi wangu, lakini nilikuwa nimehisi utupu katika nafsi yangu. Sikujua kile kingejaza shimo hilo, lakini nilihisi kuwa nilikuwa na kitu cha kufanya na familia yangu. Hapo, katika chumba cha kuunganisha familia, vitu vilianza kueleweka akilini na moyoni mwangu.

Siku chache tu, wamisionari walituongelesha tena. Wakati huu tulikuwa tunataka sana kusikiza ujumbe wao.

Wamisionari walituhimiza kuomba kila mara kuhusu ukweli. Niliamua hii ilikuwa njia pekee mimi ningeweza kuomba. Nilijuwa singefanya msimamo wa kuungana na Kanisa bila kuwa na ushuhuda wa kweli. Nilikuwa na wasi wasi wa kumjia Baba wa Mbinguni kuulizia udhibitisho kutoka Kwake, lakini wakati huo huo, nilijua angenijibu. Nilishiriki Naye matakwa ya kina ya moyo wangu na kumuuliza anipe jibu ambalo lingenihakikishia kuwa kuungana na Kanisa kulikuwa njia sahihi.

Wiki iliofuata katika Darasa la Shule ya Jumapili, rafiki yetu aliyekuwa ametualika katika ufunguzi wa hekalu alikuwa amekaa nyuma yangu. Alisonga mbele na kuanza kunizungumzia. Maneno aliyosema yalijibu kabisa kile nilichokuwa nimeomba kujua. Sikuwa na shaka kuwa Baba wa Mbinguni alikuwa akinizungumzia kumpitia Yeye. Wakati huo, nilikuwa mtu mkali, mgumu, lakini moyo wangu ukayeyuka na nikaanza kulia. Rafiki yangu alipomaliza, alialika mke wangu nami kubatizwa. Tulikubali

Mnamo Oktoba 31, 1978, chini ya mwezi moja baada ya uzoefu wetu katika hekalu la São Paulo, tulibatizwa na kudhibitishwa. Siku ya pili tulishiriki katika kikao cha pili cha kuweka wakfu hekalu la São Paulo Brazil. Mwaka moja baadaye tulirudi hekaluni na wana wetu wawili kuunganishwa pamoja kama familia. Fursa zote tatu zilikuwa za kupendeza, na uzoefu za kukumbuka. Tumeendelea kukuza hisia hizo na ibada ya hekalu ya kila mara kwa miaka mingi.

Miaka ishirini na nane tangu siku tuliobatizwa, mke wangu nami tulisimama tena katika Hekalu la São Paulo Brazil. Nilikuwa nimeitwa kama rais wa hekalu. Ilikuwa uzoefu nyeti kwetu kutembelea ukumbi wa nyumba ya Bwana na kuhisi upya hisia nyeti zilizokuwa vichocheo vya uongofu wetu.

Hekalu linaendelea kumpatia mke wangu nami furaha kuu. Tunapoona wenzi vijana wakiingia hekaluni kuunganishwa kama familia ya milele, tunahisi tumaini kuu.

Watu wengi ulimwenguni kwote wako tayari kusikiza ujumbe wa injili. Wanahisi kiu sawa na nilichohisi zaidi ya miaka 30 iliyopita. Hekalu na maagizo yake yana nguvu ya kutosha kukata kiu hicho na kujaza mashimo yao.

Picha na Laureni Fochetto