Wito na Huduma ya Yesu Kristo
Kutoka kwa hotuba ya mkutano ya ibada uliotolewa Agosti 18, 1998, Chuo Kikuu cha Brigham Young. Kwa nakala mzima katika Kingereza, nenda speeches.byu.edu.
Ushuhuda bora wa kumsujudu kwetu Yesu ni kwetu kumuiga Yeye.
Kama mmoja kati ya “mashahidi wa kipekee wa jina la Kristo duniani kote” (M&M 107:23), Ninaamini ninatumika vyema nikifundisha na kushuhudia juu Yake. Kwanza, ninaweza kuuliza swali ambalo Yeye aliuliza Mafarisayo: “Mwaonaje katika habari za Kristo? ni mwana wa nani?” (Mathayo 22:42).
Maswali haya mara nyingi huja akilini ninapokutana na viongozi wa serikali na vitengo vya dini tofauti. Wengine hukiri kuwa “Yesu alikuwa mwalimu mkuu.” Wengine husema, “Alikuwa Nabii.” Wengine tu hawamjui Yeye kamwe. Hatupaswi kushangazwa kabisa. Hata hivyo, watu wachache kiasi wako na kweli za injili ya urejesho ambazo tunazo. Washiriki wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho ni miongoni mwa wale walio wachache wanaodai kuwa Wakristo.
Hali yetu leo ilitabiriwa karne zilizopita na Nefi:
“Na ikawa kwamba niliona Kanisa la Mwanakondo wa Mungu, na hesabu yake ilikuwa chache … ; walakini nikaona kwamba kanisa la Mwanakondo, ambao walikuwa ni watakatifu wa Mungu, pia nao walikuwa kote usoni mwa dunia; na utawala wao usoni mwa dunia ulikuwa mdogo. …
“Na ikawa kwamba mimi, Nefi, niliona nguvu za Mwanakondoo wa Mungu, kwamba ziliwashukia watakatifu wa kanisa la Mwanakondoo, na kwa watu wa agano wa Bwana, ambao walitawanyika kote usoni mwa dunia; na walikuwa wamejikinga kwa utukufu na kwa nguvu za Mungu katika utukufu mkuu.” (1 Nefi 14:12, 14).
Haki hio, nguvu hio, na utukufu huo—kweli, baraka zetu zote nyingi—zinatokana na ufahamu wetu wa, utiifu kwa, na shukrani na upendo kwa Bwana Yesu Kristo.
Wakati wa safari yake fupi kiasi duniani, Mwokozi alitimiza malengo mawili makuu. Moja lilikuwa “kazi na utukufu [Wake]—kuleta kutokufa na uzima wa milele wa wanadamu” (Musa 1:39). Lingine alisema kwa urahisi: “nimewapa kielelezo, ili kama mimi ninavyowatendea, nanyi mtende vivyo” (Yohana 13:15).
Lengo Lake la kwanza tunajua kama Upatanisho. Hii ilikuwa wito Wake wa ajabu duniani. Kwa watu wa Amerika ya kale, Bwana aliyefufuka alipeana maelezo ya wito Wake:
“Nilikuja kwenye ulimwengu kufanya mapenzi ya Baba, kwa sababu alinituma.
Na Baba yangu alinituma ili nipate kuinuliwa juu kwenye msalaba; na baada ya kuinuliwa juu kwenye msalaba, kwamba ningeleta watu wote kwangu” (3 Nefi 27:13–14).
Katika kuendeleza hotuba Yake, alifunua lengo Lake la pili—kuwa kielelezo wetu: “mnajua vitu ambavyo mnahitajika kufanya … ; kwani vitendo ambavyo mmeniona nikifanya hivyo pia mtafanya” (3 Nefi 27:21).
Lengo lake la kwanza, nimeelezea kama wito Wake. Lengo Lake la pili ningependa kutambua kama huduma Yake. Wacha turejelee sehemu hizi mbili za maisha Yake—Wito na Huduma Yake.
Wito wa Yesu Kristo—Upatanisho
Wito wake ulikuwa Upatanisho. Wito huo ulikuwa ni Wake wa kipekee. Akiwa amezaliwa na mama wa kiulimwengu na Baba wa kiungu, alikuwa ndiye wa pekee ambaye angeweza kuweka maisha Yake chini kwa kujitolea na kuyachukua tena (ona Yohana 10:14–18). Matokeo matakatifu ya Upatanisho Wake yalikuwa ya daima na milele. Alichukua uchungu wa kifo na akaufanya kuwa wa muda dhiki ya kaburi (ona 1 Wakorintho 15:54–55). Jukumu lake la Upatanisho lilijulikana hata kabla ya Uumbaji na Kuanguka. Halikuwa tu la kupeana ufufuo na kutokufa kwa kila mwanadamu, lakini lilikuwa pia kutuwezesha kusamehewa dhambi zetu—kulingana na matarajio yaliyowekwa Naye. Hivyo basi Upatanisho Wake ulifungua njia ambayo tungeunganishwa Naye na familia zetu milele. Tarajio hili tunaloenzi kama uzima wa milele—zawadi kuu ya Mungu kwa mwanadamu (ona M&M 14:7).
Hakuna mwingine angeliweza kufanya Upatanisho. Hakuna mtu mwingine, hata na mali na nguvu kuu, angeweza kuokoa nafsi moja—hata yake mwenyewe (ona Mathayo 19:24–26). Na hakuna mtu mwingine binafsi atakayetarajiwa au kukubaliwa kumwaga damu kwa ajili ya uokovu wa milele wa mwanadamu mwinigine. Yesu aliifanya “mara moja tu” (Waebrania 10:10).
Ingawa Upatanisho ulitekelezwa wakati wa Agano Jipya, matokeo ya Agano la Kale kwa mara nyingi yalitabiri umuhimu wake. Adamu na Hawa waliamuriwa watoe dhabihu kama “mfano wa dhabihu ya Mzaliwa wa Pekee wa Baba” (Musa 5:7). Kivipi? Kwa kumwaga damu. Kutokana na uzoefu wao mwenyewe walidhibitisha maandiko kuwa “uhai wa mwili u katika damu” (Mambo ya Walawi 17:11).
Madaktari wanajua kuwa mara tu damu inapowacha kuenda kwa ogani, shida huanza. Kama mbubujiko wa damu kwa mguu umedakizwa, gangrini huenda ikafuatia. Kama mbubujiko kwa akili umekatizwa, upoozaji huenda ukafuatia. Kama damu imeshindwa kububujika kwa kawaida kupitia mshipa wa moyo, mshtuko wa moyo huenda ukatokea. Na ikiwa hemoraji haijazuiwa, kifu hufuatia.
Adamu, Hawa na uzao uliofuatia walijifunza kuwa wakati wowote walipomwanga damu kutoka kwa mnyama, maisha yake yalikatizwa. Kwa shughuli yao ya dhabihu, si tu mnyama yoyote angetosha. Alikuwa awe mwana-kondoo wenu atakuwa hana ila, mume wa mwaka mmoja (ona, kwa mfano, Kutoka 12:5). Matarajio haya yalikuwa pia ni ya ishara ya dhabihu itakayomtendekea Kondoo wa Mungu asiye na ila.
Adamu na Hawa walipewa amri: “Kwa hiyo, nawe utafanya yale yote uyafanyayo katika jina la mwana, nawe utatubu na kumlingana Mungu katika jina la Mwana milele yote” (Musa 5:8). Tangu siku hiyo hadi katika meridiani ya siku, dhabihu ya mnyama iliendelea kuwa kielelezo na kivuli cha Upatanisho utakaotendeka wa Mwana ya Mungu.
Wakati upatanisho ulikamilishwa, dhabihu hio kuu na wa mwisho ilitekeleza amri ya Musa (ona Alma 34:13–14) na ikamaliza (Mambo ya Walawi 17:11). Yesu alieleza jinsi vipengee vya dhabihu ya kale vilitekelezwa na Upatanisho na kukumbukwa kiashiria na sakramenti. Zingatia tena rejeleo kwa maisha, mwili na damu.
“Basi Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambieni, Msipoula mwili wake Mwana na Adamu na kuinywa damu yake, hauna uzima ndani yenu.
“Aulaye mwili wangu, na kuinywa damu yangu, anao uzima wa milele; nami nitamfufua siku ya mwisho” (Yohana 6:53–54).
Kwa sababu ya Upatanisho wa Yesu Kristo, kila mwanadamu—hata kwa wengi watakao—wataokolewa. Mwokozi alianza kumwaga damu Yake kwa wanadamu wote si kwa msalaba lakini katika ya Bustani la Gethsemani Pale alichukua juu Yake uzito wa dhambi za dunia ya wote waliowahi kuishi. Chini ya mzigo huo mzito, alitokwa damu kwenye kila kinyweleo (ona M&M 19:18). Mateso ya Upatanisho yalimalizwa kwenye msalaba Kalivari.
Umuhimu wa Upatanisho ulifupishwa na Nabii Joseph Smith. Alisema “Kanuni za msingi za dini yetu ni ushuhuda wa Mitume na Manabii, kuhusu Yesu Kristo, kwamba alikufa, akazikwa, na akafufuka tena siku ya tatu, na kupaa mbinguni; na mambo yote mengine ambayo yanahusiana na dini yetu ni viambatisho tu”1
Na mamlaka haya na shukrani ya dhati, Ninafundisha na kushuhudia juu Yake.
Huduma ya Yesu Kristo—Mfano
Lengo la Bwana la pili la thamani sana duniani ilikuwa kushiriki kama mfano kwetu. Maisha yake ya mfano yalijumuisha huduma Yake duniani. Yalijumuisha mafundisho Yake, mifumbo na hotuba. Yalijumuisha Miujiza Yake, upendo mkarimu, na subira kwa watoto wa watu (ona 1 Nefi 19:9). Yalijumuisha matumizi Yake ya huruma ya mamlaka ya ukuhani. Yalijumuisha haira Yake ya haki aliposhutumu dhambi (ona Warumi 8:3) na alipotupilia meza ya wabadilishaji pesa (ona Mathayo 21:12). Yalijumuisha pia huzuni Wake mkubwa. Alifanyiwa mzaha, na kupigwa, na kukataliwa na watu Wake mwenyewe (ona Mosia 15:5)—hata kusalitiwa na mfuasi mmoja na kukataliwa na mwingine (ona Yohana 18:2–3, 25–27).
Hata vile vitendo vyake vya huduma vilikuwa vya kushangaza, havikuwa na bado si vya kipekee Kwake. Hakuna kipimo cha idadi ya watu ambao wanaweza kufuata mfano wa Yesu. Vitendo sawa na hivyo vimetendwa na manabii Wake na mitume na wengine miongoni mwa washiriki Wake walio na mamlaka. Wengi wamevumilia mateso kwa ajili Yake (ona Mathayo 5:10; 3 Nefi 12:10). Katika wakati wetu, unajua akina ndugu na dada ambao wamevumilia kwa dhati—hata kwa matokeo mabaya—kuiga mfano wa Bwana.
Hivyo ndivyo inapaswa kuwa. Hiyo ndiyo tumaini Lake kwetu. Bwana anatuomba tufuate mfano Wake. Maombi yake yako wazi kabisa:
-
“Mnapaswa kuwa watu wa aina gani? … Hata vile nilivyo, (3 Nefi 27:27; ona pia 3 Nefi 12:48).
-
“Nifuateni, nami nitawafanya kuwa wavuvi wa watu” (Mathayo 4:19).
-
“Nimewapa kielelezo, ili kama mimi nilivyowatendea, nanyi mtende hivyo” (Yohana 13:15; ona pia Yohana 14:6).
Haya na maandiko mengine hayakuandikwa kama mapendekezo. Ni amri tukufu! Tunapaswa tuige mfano Wake!
Ili kusaidia matakwa yetu ya kumfuata Yeye, pengine tungezingatia vipengele vitano vya maisha Yake ambavyo tunaweza kuiga.
Upendo
Ikiwa tungeuliza ni sifa gani ya maisha Yake ungetambua kwanza, ninadhani ungetaja sifa Yake ya upendo. Hiyo ingejumuisha huruma, ukarimu, wema, fadhili, uchaji Mungu, buraa, rehema, haki na mengine. Yesu aliwapenda Baba na mama Yake (ona Yohana 19:25–27). Alipenda familia Yake na Watakatifu (ona Yohana 13:1; 2 Wathesalonike 2:16). Alimpenda mtenda dhambi bila kukubali dhambi (ona Mathayo 9:2; M&M 24:2). Na alitufunza jinsi tunaweza kuonyesha upendo wetu Kwake. Alisema, “Mkinipenda, mtazishika amri zangu (Yohana 14:15). Kisha, ilikusisitiza kuwa upendo wake haukuwa bila matarajio, aliongezea, “Mkizishika amri zangu, mtakaa katika upendo wangu; kama vile mimi nilivyozishika amri za Baba yangu na kukaa katika pendo lake” (Yohana 15:10; ona pia M&M 95:12; 124:87).
Dhihirisho lingine la upendo wa Mwokozi ilikuwa utumishi Wake. Alitumikia Baba Yake, na alitumikia watu ambao aliishi nao na kufanya kazi nao. Kwa njia zote mbili tunapaswa tuige mfano Wake. Tunapaswa tumtumikie Mungu, “kwenda katika njia zake zote, na kumpenda” (Kumbukumbu la Torati 10:12; ona pia 11:13; Yoshua 22:5; M&M 20:31; 59:5). Na tunapaswa tupende majirani wetu kwa kuwatumikia (ona Wagalatia 5:13; Mosia 4:15–16). Tunaanza na familia zetu. Upendo wa kina unaoshikanisha wazazi kwa watoto wao unaendelezwa kwa utumishi kwao katika wakati wao wa utegemeo kamilifu. Baadaye maishani watoto watiifu wanaweza kuwa na nafasi ya kulipiza upendo huo wanapotumikia wazazi wao wakongwe.
Maagizo
Kipengele cha pili cha mfano ya Mwokozi kilikuwa usisitizo Wake wa maagizo matakatifu. Wakati wa huduma Yake duniani alionyesha umuhimu wa maagano ya wokovu. Alibatizwa na Yohana katika Mto Jordan. Hata Yohana aliuliza, “Kwa nini?”
Yesu alieleza, Kwa kuwa ndivyo itupasavyo sisi kuitimiza haki yote” (Mathayo 3:15; sisitizo limeongezwa). Agizo halikuwa tu muhimu, ila mfano uliowekwa na Yesu na Yohana ulikuwa pia muhimu.
Baadaye Bwana alianzisha agizo la sakramenti. Alieleza ishara ya sakramenti na kutoa nembo zake tukufu kwa wafuasi Wake (ona Mathayo 26:26–28; Marko 14:22–24; Luka 24:30).
Baba yetu wa Mbinguni alipeana maelezo pia kuhusu maagizo. Alisema: “Lazima mzaliwe tena katika ufalme wa mbinguni, kwa maji na kwa Roho, na kuoshwa kwa damu, hata damu ya Mwanangu wa Pekee; ili mpate kutakaswa kutokana na dhambi zote, na kufurahia maneno ya uzima wa milele katika ulimwengu huu, na uzima wa milele katika ulimwengu ujao, hata utukufu katika mwili usiokufa” (Musa 6:59).
Wakati wa shughuli za Bwana za baada ya muda duniani, maagizo ya juu ya wokovu yalifunuliwa (M&M 124:40–42). Amewezesha kwa ajili ya maagizo haya katika mahekalu Yake matukufu. Katika siku zetu, miosho, mitakaso, na miakifisho yanapewa kwa watu binafsi ambao wamejitayarisha vizuri (ona M&M 105:12, 18, 33; 110:9; 124:39). Hekaluni, mtu binafsi aweza kuunganishwa na bwana ama mke, kwa wakongwe, na kwa uzao (ona M&M 132:19). Msimamizi wetu ni Mungu wa sheria na mpangilio (ona M&M 132:18). Lengo lake kwa maagizo ni sehemu kuu ya mfano Wake kwetu.
Maombi
Kipengele cha tatu cha huduma ya mfano wa Bwana ni maombi. Yesu aliomba kwa Baba Yake wa Mbinguni na pia alitufundisha jinsi ya kuomba. Tunapaswa tuombe kwa Mungu Baba wa Milele katika jina la Mwana Wake, Yesu Kristo, kupitia uwezo wa Roho Mtakatifu (ona Mathayo 6:9–13; 3 Nefi 13:9–13; Tafsiri ya Joseph Smith, Mathayo 6:9–15). Ninapenda Maombi Makuu ya Upatanisho yaliyotolewa na Bwana yaliyorekodiwa katika Yohana, sura ya 17. Ndani yake Mwana anazungumza wazi na Baba Yake kwa niaba ya wafuasi Wake, ambao Yeye anawapenda. Ni mfano wa maombi ya kufaa na ya huruma.
Maarifa.
Kipengele cha nne cha mfano wa Bwana ni matumizi ya maarifa Yake matukufu. Kama ilivyorejelewa awali, wengi wasio Wakristo walikiri kuwa Yesu alikuwa mwalimu bora. Kweli, Alikuwa Lakini ni nini kilitofautisha mafundisho Yake? Je, alikuwa ni mwalimu hodari wa uhandisi, hesabu au sayansi? Kama Muumbaji wa dunia hii na mengine (ona Musa 1:33), kwa kweli angekuwa. Ama, kama Mbuni wa maandiko, angefundisha ubuni wa maandishi vizuri sana.
Sifa inayotofautisha mafundisho Yake juu ya yale yote ya walimu wengine ilikuwa ni kuwa alifundisha ukweli wa umuhimu wa milele. Ni Yeye pekee yake ndiye angeweza kutufunulia lengo letu maishani. Ni kumpitia Yeye pekee ndiko tungeweza kujifunza maisha kabla ya maisha duniani na uwezo wetu wa maisha baada ya maisha duniani.
Wakati mmoja Mwalimu Bora aliwaambia wasikilizaji wake walioshuku kuwa wako na shuhuda tatu juu Yake:
-
Yohana Mbatizaji
-
Matendo ambayo yesu alikuwa amekamilisha.
-
Neno la Mungu Baba wa Milele (ona Yohana 5:33–37).
Kisha akatoa shahidi nne: “Mwayachunguza maandiko; kwa sababu mnadhani ninyi mna uzima wa milele ndani yake: na hayo ndiyo yanayonishuhudia” (Yohana 5:39).
Neno dhani katika fungu hilo linaweza kwa mara ya kwanza kuonekana kuwa mahali halifai. Lakini ni muhimu kwa ajili ya maana Yesu alikuwa anajaribu kueleza. Alijua kuwa wengi wa wasikilizaji Wake bayana walidhania kuwa maisha ya milele yalikuwa katika maandiko. Lakini walikosea. Maandiko pekee yake hayawezi kupeana maisha ya milele. Kwa kweli kuna nguvu katika maandiko, lakini nguvu hiyo huja kutoka kwa Yesu Mwenyewe. Yeye ndiye Neno: Logos. Nguvu ya uzima wa milele zi ndani Yake, ambaye “hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye neno alikuwa Mungu” (Yohana 1:1; ona pia 2 Nefi 31:20; 32:3). Kisha, kwa sababu ya ungumu wa wenye kushuku Wake, Yesu aliendelea kuwashutumu: “Wala hamtaki kuja kwangu mpate kuwa na uzima [wa milele]” (Yohana 5:40).
Bwana angetushinda na maarifa Yake ya kiungu, lakini hafanyi hivyo. Anaheshimu wakala wetu. Anaturuhuru furaha wa kugundua. Anatuhimiza kutubu makosa yetu wenyewe. Anaturuhusu kuwa na uzoefu wa uhuru unaokuja kutokana na kutaka kwetu kutii sheria Zake tukufu. Ndio, njia anayotumia maarifa Yake inatupatia sisi mfano mkuu.
Uvumilivu
Kipengele cha tano ya uchungaji wa Bwana ni msimamo wake wa kuvumilia hadi mwisho. Katu hakujitoa kutoka kwa uteuzi Wake. Ingawa alipitia mateso zaidi ya yale tunayoweza kutafakari, hakuwa wa kulegea. Kupitia majaribio ya kina alivumilia hadi mwisho wa jukumu Lake: kulipia kosa kwa ajili ya dhambi ya wanadamu wote. Maneno Yake ya mwisho aliponing’inia msalabani yalikuwa, “Imeisha” (Yohana 19:30).
Matumizi Maishani Mwetu
Vipengele hivi vitano vya huduma Yake vinaweza kutumika maishani mwetu wenyewe. Kwa kweli shuhuda bora za kusujudu kwetu Yesu ni kwetu kumuiga.
Tunapoanza kufahamu Yesu ni nani na kile ambacho ametutendea, tunaweza kuelewa, kwa kiwango fulani, mantiki ya amri ya kwanza na kuu: “Nawe mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote, na kwa nguvu zako zote” (Marko 12:30). Vingine, yote tunayofikiri na kutenda na kusema yapaswa yaloweshwe katika upendo wetu Kwake na Baba Yake.
Jiulize, “Kunaye yeyote ninayempenda zaidi ya Bwana?” Kisha linganisha jibu lako na viwango vilivyowekwa na Bwana:
-
“Apendaye baba au mama kuliko mimi, hanistahili”
-
“Ampendaye mwana au binti kuliko mimi, hanistahili” (Mathayo 10:37).
Upendo kwa familia na marafiki, hata kwa uzuri wake wote, ni wa kiini zaidi wakati unadhibitishwa katika upendo wa Yesu Kristo. Upendo wa wazazi kwa watoto una maana zaidi hapa na baadaye kwa sababu Yake. Mahusiano yote ya mapenzi yanatukuzwa katika Yeye. Upendo wa Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo unatupa mwangaza, uvutio na ushawishi kuwapenda wengine kwa njia bora zaidi.
Maagizo hutupa fokasi ya utumishi wa umuhimu wa milele. Wazazi wanapaswa wazingatie ni agizo gani linahitajika kufuatia kwa kila mtoto. Walimu wa nyumbani wanapaswa wafikirie kuhusu agizo la kufaa linalohitajika kufuatia katika kila familia wanaotumikia.
Mfano wa Mwokozi wa maombi unatukumbusha kuwa maombi ya kibinafsi, maombi ya familia, na utekelezaji wa uteuzi wetu katika Kanisa kwa maombi unapaswa kuwa sehemu ya maisha yetu. Kujua na kufanya matakwa ya Baba hutupa uwezo mkuu wa kiroho na kujiamini (ona M&M 121:45). Kwenye upande wa Bwana ndipo tunataka kuwa.
Maarifa “kuhusu vile vitu vilivyo, na vile vitu vitavyokuwa” (Yakobo 4:13) yanatukubalisha kutenda juu ya kanuni za kweli na mafundisho. Maarifa hayo yatainua kiwango chetu cha tabia. Vitendo ambavyo vingependekezwa na hamu na hisia vitashindwa na vitendo vilivyoundwa na mantiki na haki.
Msimamo wa kuvumilia hadi mwisho humaanisha kuwa hatutauliza kutolewa katika wito wa kuhudumu. Humaanisha kuwa tutavumilia katika kufuatilia lengo la kustahili. Humaanisha kuwa hatutawai kukata moyo kwa ajili ya mpendwa ambaye amepotoka. Na humaanisha kuwa daima tutatunza mahusiano yetu ya milele ya familia, hata wakati wa shida ya ugonjwa, ulemavu au kifo.
Kwa moyo wangu wote ninaomba kuwa ushawishi unaobadilisha wa Bwana uweze ukalete tofauti ya kina katika maisha yako. Wito Wake na huduma Yake iweze kubariki kila moja wetu na milele na milele.