2013
Ukuaji katika Udongo wa Rutuba: Vijana Waaminifu nchini Uganda
Aprili 2013


Ukuaji katika Udongo wa Rutuba: Vijana WAAMINIFU nchini Uganda

Cindy Smith aliishi nchini Uganda wakati mumewe alifanya kazi huko, na sasa wanaishi Utah, Marekani.

Wanapokubali na kuishi Injili ya Yesu Kristo, vijana nchini Uganda wanaona imani na tumaini likukua kwote karibu nao.

Katikati mwa Afrika Mashariki, nchi nzuri ya Uganda imebarikiwa na milima mingi yenye miwa na migomba ya ndizi—na vijana waliotayari kukubali na kuishi Injili ya Yesu Kristo.

Kigingi cha kwanza Uganda kiliundwa mwaka 2010. Kanisa linakua kwa kasi, na wavulana na wasichana wengi katika kila kata na tawi.

Kupandisha Bendera, Kuwa Mfano

Wasichana katika kata moja walivutiwa na mafundisho ya Dada Elaine S. Dalton, Rais Mkuu wa Wasichana, juu ya wema: “Sasa ni wakati kwa kila mmoja wetu kuinuka na kupeperusha bendera kwa kuita ulimwengu kurudi kwa wema.”1 Wasichana walipanda mlima ulio juu ya mji na kuinua bendera za dhahabu kuashiria ahadi zao za kuwa mifano wa wema. Pamoja waliimba “High on the Mountain Top” (Wimbo, nambari. 5).

Wasichana hawa wamepandisha viwango vyao vya kibinafsi vya haki. Utiifu wao umeimarisha ushahidi wao na kushawishi wengine. Dada Dalton amesema, “Kamwe usiwaikudharau nguvu za ushawishi wako wa wema”2 Na kama bendera, mfano wa wasichana hawa unapepea ulimwenguni kote.

Sandra

Kama wasichana wengi nchini Uganda, Sandra hutembea zaidi ya maili kuenda kanisani, husaidia kusafisha kanisa siku ya Ijumaa, na huhudhuria seminari Jumamosi. Wakati wa wiki, yeye huamka kabla ya 11:00 asubuhi kusoma vitabu vya shuleni, na kisha hutembea kuenda shule, kurudi nyumbani baada ya saa 12:00 jioni. Alikosa mwaka wa shule kwa sababu ya matatizo ya kifedha lakini hukumbana na changamoto yake kwa mtazamo mzuri: “injili kwa kweli imenisaidia kukaa imara na kutohamishika.”

Sandra ni mshiriki wa pekee wa Kanisa katika familia yake, lakini wazazi wake husaidia huduma yake ya Kanisa, kama vile kusaidia wakati kata ilisafisha viwanja vya watoto mayatima mtaani. Familia yake huona jinsi injili imemsaidia kuwa na nguvu, hata wakati anakabiliwa na matatizo ambayo hayajasuluhishwa. Akitafakari juu ya chanzo cha nguvu hio, Sandra anasema, “Ninapoenda Kanisani, ninajisikia kama ninavalia silaha za Mungu” (ona Waefeso 6:11–17).

Mwongofu wa hivi karibuni, Susan, analipenda Kanisa. Mzaliwa kutoka Sudan Kusini, familia yake ilikimbia taabu na ikabarikiwa kupokea wamisionari katika Uganda. Kama mkimbizi, alipata amani na ulinzi katika Injili. Siku za Jumapili angewaleta ndugu zake wadogo kanisani, na pia watoto wengine 10 ambao si washiriki wa Kanisa. Baada ya kifo ghafula cha mwana familia, alirudi Sudan Kusini, ambapo anasubiri Kanisa liundwe katika eneo lake. Susan na Sandra wote wanakumbana na changamoto, lakini wanategemea Mungu na kufurahia matunda ya kuishi Injili ya Yesu Kristo (ona Alma 32:6–8, 43).

Kujitolea Kuhudumu katika Misheni

Vijana nchini Uganda huanza kucheza kandanda kama wavulana wadogo, wakitumia matawi ya yaliyofumwa kama mpira. Tangu alipokuwa mdogo sana, Dennis alikuwa na kipaji cha mchezo, na shule yake ya sekondari ilimpa udhamini ili kuchezea timu yao. Baada ya kumaliza shule ya sekondari, timu ya kulipwa ilimpa malipo, chumba, na malazi. Ilikuwa ni ndoto ya kuwa kweli, lakini Dennis alijua hii ingeharibu mipango yake ya kwenda misheni baadaye katika mwaka.

Dennis

Hamu ya Dennis kufanya kile Baba yake wa Mbinguni alimtaka afanye ilikuwa kubwa sana kana kwamba hakutaka hata kujaribiwa kubaki katika timu wakati ungefika kwake kushiriki misheni. Watu wengi walihoji uchaguzi wake, lakini Dennis yu dhabiti kuwa alifanya uamuzi wa haki—kwa ajili yake mwenyewe na wengine. “Ndugu zake wawili wadogo na dadake mdogo walibatizwa,” anasema. “Sikuwai kamwe kufikiria kuwa dadangu angesikia Injili. Ninapomuona Mungu akifanya miujiza katika familia yangu, inanipa matumaini kwa ajili ya siku zangu za usoni.”

Katika kata ya Dennis wavulana hujifunza Hubiri Injili Yangu kila wiki. Wamekuwa kama timu, wakifanya kazi kwa karibu na wamisionari wa muda na kuleta marafiki kwa mikutano ya Jumapili na shughuli zingine, ikiwa ni pamoja na mpira wa kikapu na michezo ya kandanda wakati wa wiki. Makuhani wamewabatiza marafiki na wengine walisaidia kuwafunza pamoja na wamisionari. Zaidi ya miaka kadhaa, timu hii ya vijana imeimarisha kata nzima, na wanne wao, ikiwa ni pamoja na Dennis, walipokea wito kuenda katika Misheni ya Kenya Nairobi.

Wamefuata ushauri wa Mzee Daudi A. Bednar wa Jamii ya Mitume Kumi na Wawili “kuweni wamisionari kitambo kabla mwasilishe makaratasi yenu ya misheni.”3 Walifanya hivyo kwa kufanya kazi pamoja kama jamii, timu bora kuliko yoyote nyingine.

Wamisionari wote wanne walishinda changamoto ili kuhudumu. Wilberforce anaelezea, “Nilikuwa karibu kupoteza matumaini ya kwenda misheni kwa sababu ya gharama, lakini basi nikasoma Mathayo 6:19–20: ‘Usijiwekee hazina duniani lakini jiwekeeni hazina wenyewe mbinguni.’ Kwa hivyo kwa bidii na kujitolea, niliweza kutimiza lengo langu la kuhudumu misheni ya muda. Naipenda huduma ya umisionari. Hakuna kilicho bora kuliko kutafuta kwanza ufalme wa mbinguni.”

Matumaini kwa Siku za Usoni

Vijana wa Uganda wanasaidia kujenga ufalme wa Mungu hapa, na tumaini kubwa kwa ajili ya siku zijazo. Ingawa hakuna hekalu Afrika Mashariki, vijana huangazia wakati wataoa katika hekalu lililo mbali. Shughuli moja ya kigingi ililenga kujiandaa kuingia hekaluni, na katika hitimisho, mshiriki wa urais wa kigingi akatoa ushuhuda wake: “Mungu anawapenda. Nyinyi ndio siku za usoni za Kanisa nchini Uganda.” Vijana hawa wenye haki tayari wana ushawishi mkubwa.

Wavulana na wasichana wa Uganda wanaacha mambo ya dunia kwa ajili ya baraka ambazo zitadumu milele. Wamepanda mbegu ya imani na wanailisha na kuitunza (ona Alma 32:33–37). Kama mti uliojaa na matunda (ona Alma 32:42), vijana hushiriki furaha ya injili katika nchi hii yenye rutuba.

Muhtasari

  1. Elaine S. Dalton, “A Return to Virtue,” Liahona, Nov. 2008, 80.

  2. Elaine S. Dalton, Liahona, Nov. 2008, 80.

  3. David A. Bednar, “Becoming a Missionary,” Liahona, Nov. 2005, 45.

Juu: Vijana wanahudhuria ibada ya kigingi pamoja

Juu: Susan (katikati), mkimbizi nchini Uganda, alipata amani katika Injili na aliwaleta ndugu zake na watoto wengine kanisani.

Katikati: Wasichana wa kata hii wanafurahia kazi ya Maendeleo ya Kibinafsi.

Kulia: Dennis aliwachana na timu ya kadanda ya kulipwa ili kuhubiri Injili. Yeye na vijana wengine katika jamii yake ya ukuhani walijitolea na kushinda changamoto ili kuhudumu misheni.

Picha na Cindy Smith