2013
Maswali na Majibu
Aprili 2013


Maswali na Majibu

Je, ninawezaje kueleza rafiki yangu kuwa kuvunja sheria ya usafi wa kimwili ni wazo baya?

Baba wa Mbinguni anataka tuwe na furaha na wakustahili Roho Wake, hivyo basi Anatupatia amri kutusaidia kuweka mawazo yetu, maneno, na vitendo ndani ya mipaka sahihi. Sheria ya usafi “wa kiwili husaidia kuweka nguvu za uzazi ndani ya mipaka ya ndoa. Sababu moja Yeye hutuamuru kwamba nguvu ya uzazi itumike tu kati ya mume na mke ni kwa sababu watoto wana haki ya kuzaliwa ndani ya vifungo vya ndoa.”1

Unaweza kushiriki nakala ya Kwa Nguvu ya Vijana na rafiki yako. Inatoa sababu kadhaa kwa nini ni vizuri kuweka sheria ya usafi wa kiwili: “Wakati wewe u msafi kimaadili ya kujamiiana, unajiandaa kufanya na kushika maagano matakatifu katika hekalu. Unajitayarisha kujenga ndoa imara na kuleta watoto ulimwenguni kama sehemu ya familia ya milele na familia ya upendo. Unajikinga kutokana na uharibifu wa kiroho na kihisia ambao huja kwa kushiriki urafiki wa kujamiiana nje ya ndoa. Unajikinga pia dhidi ya magonjwa hatari. Kubaki msafi kimaadili ya kujamiiana hukusaidia kuwa na ujasiri na furaha ya kweli na huboresha uwezo wako wa kufanya maamuzi mazuri kwa sasa na baadaye.”2

Hekalu

Baba yetu wa Mbinguni ana madhumuni tukufu kwetu sisi sote, na kusudi hilo linaweza kutimizwa katika hekalu. Tunapaswa tuwe wa kustahili kuingia hekaluni ili familia zetu ziweze kufunganishwa milele. Tutaishi na Baba yetu wa Mbinguni tena, na muhimu zaidi tutakuwa na furaha isiyo na mwisho, ambayo wasiostahili hawezi kuwa nayo.

Alofa M., umri miaka 18, Samoa

Ndoa na Familia

Tunahimizwa kuwa wasafi kimaadili ya kujamiiana ili tuweze kuwa wa kustahili kuingia hekaluni na kushika maagano matakatifu. Tukifuata sheria ya usafi wa kimwili, tunaweza kujenga ndoa imara na familia katika siku zijazo. Shetani daima atatujaribu, lakini kupitia maombi, maandiko, na marafiki wema, tunaweza kushinda.

Resty M., umri miaka 16, Philippines

Matokeo Mabaya

Kuna matokeo mengi mabaya kwa kuvunja sheria ya usafi wa kimwili, lakini si yote unajifunza kuhusu katika darasa la afya. Kuvunja sheria ya usafi wa kimwili kunaweza kufukuza Roho nje ya maisha yako, kuumiza wale walio karibu nawe, na kufanya kujisikia vibaya kuhusu wewe mwenyewe. Ninapendekeza kutazama video ya Jumbe za Wamormoni iitwayo: “Usafi? Je, Ni nini Mipaka” [katika youth.lds.org katika Kiingereza, Kireno, na Kihispania].

Matthew T., umri miaka 17, Utah, USA

Usafi na Heshima

Kwa kufuata sheria ya usafi wa kimwili, tunabaki wasafi mbele ya Mungu, tunajiheshimu, na tunawasaidia wengine kutuheshimu pia. Tukitii sheria ya usafi wa kimwili, tunaonyesha kwamba sisi ni watoto wa Mungu na kwamba tunazingatia viwango vya juu. Tutaepuka majuto. Tunapotii Baba yetu wa Mbinguni, hasa kuhusu sheria hii, maisha yetu yatakuwa ya furaha zaidi hapa duniani na katika ulimwengu ujao.

Alyana G., umri miaka 19, Philippines

Kipawa Kitakatifu

Ikiwa kipawa cha uzazi kitadharauliwa, kipawa hiki cha thamani kutoka kwa Mungu kingetendewa vibaya kama kitu cha kawaida. Kutoa kipawa haihisi kuridhisha kama mtu unayempa hadhani ni maalum. Mmoja lazima daima atumie kipawa cha uzazi kwa utakatifu; kwa kuwa sisi sote ni mahekalu ya Mungu na tunapaswa tubaki wasafi kama hekalu.

Jaron Z., umri miaka 15, Idaho, USA

Roho kuwa Nasi

Unapobaki kuwa msafi kutokana na dhambi, utakuwa mwenye furaha sana na utabarikiwa. Miili yetu ni kama mahekalu, na Baba wa Mbinguni haishi katika mahekalu yaliyo machafu (Alma 7:21). Kwa hivyo tunapobaki kuwa wasafi kutokana na dhambi, Roho anaweza kuishi nasi.

Maryann P., umri miaka 14, Arkansas, USA

Maswali Muhimu

Jibu swali la rafiki yako kwa kuuliza baadhi ya maswali: “Je, kama mwenzi wako wa siku zijazo angekuwa anakutazama wewe sasa?” Watu wote nimesikia kuhusu ambao wamevunja sheria ya usafi wa kimwili wamejuta kufanya hivyo. “Je, kama mtoto wako wa siku zijazo akikuuliza kama umevunja sheria ya usafi wa kimwili?” Rafiki yako anahitaji kujifunza jinsi sheria ya usafi wa kimwili ni muhimu sasa, kabla ya mwana au binti aulize swali hilo. Unahitaji kujiweka kuwa msafi na hasili ili kuwa na maisha ya furaha, afya bila hatia ya kuvunja sheria takatifu.

Robyn K., umri miaka 13, Utah, USA

Wema na Usafi

Bwana hufurahia wema na usafi wa kimwili, na kila kitu kinapaswa kufanyika kwa wakati wake ufaao. Sheria ya usafi wa kimwili ni amri kutoka kwa Bwana. Maombi na uenzi wa Roho ni mchanganyiko kamili wa kujua kwamba kuwa msafi kimwili ni baraka.

Selene R., umri miaka 18, Nicaragua

Katika Ndoa

Ningemuelezea rafiki yangu kwamba kuvunja sheria ya usafi wa kimwili ni wazo baya kwa sababu nguvu ya uzazi imetengenezewa waliooana kisheria. Tunapovunja sheria ya usafi wa kimwili, tunapoteza Roho Mtakatifu katika maisha yetu.

Augustina A., umri miaka 15, Ghana

Muhtasari

  1. Familia: Tangazo kwa Ulimwengu, Liahona, Nov. 2010, 129.

  2. Kwa Nguvu ya Vijana (kijitabu, 2011), 35.