2020
Miaka 200 ya Nuru
Aprili 2020


Miaka 200 ya Nuru

First Vision

Siku moja nzuri, angavu miaka 200 iliyopita, mvulana mmoja aliingia katika msitu akiwa na nia ya kutafuta msamaha na kusali kuhusu kanisa ambalo angejiunga nalo. Kutokana na ono la kimiujiza, alijifunza kwamba asijiunge na lolote. Hivyo kuashiria mwanzo wa Urejesho wa injili ya Yesu Kristo—mchakato ambao unaendelea katika siku yetu.

Katika toleo hili, tunasherehekea miaka 200 ya Nuru:

  • Rais Russell M. Nelson anafundisha jinsi kukusanya Israeli kutoka pande zote mbili za pazia kunavyoweza kututayarisha sisi pamoja na wengine kwa ajili ya Ujio wa Pili wa Bwana (ukurasa wa 6).

  • Mzee LeGrand R. Curtis Jr. anaonesha jinsi ambavyo Watakatifu wa Siku za Mwisho wamechangia kwenye Urejesho unaoendelea—na jinsi kila mmoja wetu anavyoweza kuchangia (ukurasa wa 18).

  • Kwa ajili ya vijana, Mzee Neil L. Andersen anashiriki kweli tano tunazoweza kujifunza kutokana na Ono la Kwanza (ukurasa wa 52).

Tunapojifunza kutoka kwenye maneno ya nabii wetu na hadithi za Watakatifu waaminifu, na tuweze kuja kwenye ufahamu sawa na ule ambao Nabii Joseph alipata kuelewa miaka 200 iliyopita: kwamba Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo ni viumbe wa kweli, wanaoishi ambao wanatupenda. Na tushiriki ufahamu huo pamoja na marafiki na majirani zetu.

Wenu waaminifu,

Mzee Randy D. Funk wa Sabini

Mhariri wa Magazeti ya Kanisa