2020
Hujambo kutoka katika Msitu Mtakatifu
Aprili 2020


Hujambo kutoka Msitu Mtakatifu!

Hello from the Sacred Grove

Habari, sisi ni Margo na Paolo.

Mwezi huu, ili kusherehekea Urejesho, tunatembelea eneo ambapo Ono la Kwanza lilitokea miaka 200 iliyopita!

Wakati Joseph Smith alipokuwa na umri wa miaka 14, aliishi katika nyumba ya magogo New York, Marekani. Alikuwa na kaka watano na dada watatu. Aliwatii wazazi wake na alikuwa mwema kwa wengine. Alisoma Biblia pamoja na familia yake, lakini wote hawakushiriki kanisa moja.

Joseph alikuwa mchapa kazi. Alisaidia kukata miti ili familia yake iweze kupanda mazao. Pia aliisaidia familia yake kukusanya utomvu kutoka kwenye miti ya maple ili kutengeneza sukari.

Joseph alitaka kupata Kanisa kama lile la kwenye Biblia. Siku moja alienda katika msitu na kusali. Baba wa Mbinguni na Yesu walimtokea. Walimwambia dhambi zake zilikuwa zimesamehewa. Pia walimwambia kwamba asijiunge na kanisa lolote. Punde Kanisa la Yesu Kristo lingerejeshwa!

Watu wengi walimfanyia mzaha Joseph kwa ajili ya kile alichoona. Walisema alikuwa akidanganya. Lakini Joseph aliendelea kusema ukweli. Alisema “Nami najua hivyo, nami nilijua kwamba Mungu alijua, na sikuweza kukataa” (Historia ya—Joseph Smith 1:25).

Leo watu wanaweza kutembelea eneo ambapo Joseph alisali. Ni zuri na la amani.

Watoto hawa wanaishi mahali alipolelewa Joseph Smith!

Ninajua Msitu Mtakatifu ni mahali maalum kwa sababu Joseph Smith alisali na kuwaona Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo pale.

Piper D., miaka 5, New York, Marekani.

Nina shukrani kwamba tunaishi karibu na nyumbani kwa Joseph Smith. Ninapenda kwenda katika Jengo la Grandin ambalo lina mtambo wa kupiga chapa. Ninapenda sana kuona mahali ambapo walijalidi nakala za mwanzo za Kitabu cha Mormoni.

Roscoe B., miaka 9, New York, Marekani

Asante kwa kutalii Msitu Mtakatifu pamoja nasi. Tutaonana wakati mwingine!

Picha za wavulana na Julie Poulson; vielelezo na Katie McDee