2020
Kanisa la Yesu Kristo Limerejeshwa
Aprili 2020


Kanisa la Yesu Kristo Limerejeshwa!

children looking at sky

Kabla ya kuja duniani, tuliishi pamoja na Wazazi wa Mbinguni. Walitupenda! Baba wa Mbinguni alikuwa na mpango wa kupendeza kwa ajili yetu. Tungekuja duniani ili tuweze kupata mwili na kujifunza na kukua. Kisha tungeweza kurudi kuishi nyumbani kwetu mbinguni. Lakini hatungeweza kufanya hivyo peke yetu. Tungehitaji usaidizi.

Jesus reaching out to man

Baba wa Mbinguni alimchagua kaka yetu mkubwa, Yesu Kristo, aje duniani kutusaidia. Yesu alituonesha jinsi ya kuwapenda wengine na kufuata amri za Baba wa Mbinguni. Aliwachagua Mitume waliongoze Kanisa Lake.

girl looking out the window

Yesu Aliteseka kwa ajili yetu katika Bustani ya Gethsemane. Alihisi uchungu na huzuni yetu yote. Alikufa msalabani kwa ajili yetu. Kwa sababu ya hili, tunaweza kwenda Kwake wakati tumeumia au tuna huzuni au tunahitaji msaada. Tunaweza kutubu wakati tunapofanya makosa.

Jesus and Mary at the tomb

Siku ya tatu baada ya Yesu kufa, alifufuka. Yesu alikuwa hai tena! Kwa sababu hili, sisi pia tutafufuliwa. Tunaweza kuishi mbinguni tena baada ya sisi kufa.

girl getting baptized

Baada kufufuka Kwake, Yesu aliwatembelea wafuasi Wake huko Amerika. Aliwaomba Mitume Wake waendelee kufundisha watu kuhusu injili Yake. Watu wengi waliowasikiliza Mitume walibatizwa na kujiunga na Kanisa.

man with hand on his head

Baada ya Mitume kufariki, watu walianza kusahau baadhi ya vipengee muhimu vya injili ya Yesu. Waliacha kuamini kwamba Baba wa Mbinguni siku zote angewavuvia watoto wake duniani. Walisahau kwamba kila mtu duniani angekuwa na nafasi ya kubatizwa. Waliacha kuamini kwamba manabii na mitume daima wangeongoza Kanisa.

Joseph Smith

Miaka mingi ilipita. Hatimaye, ilifika wakati wa kurudisha vipengee vilivyopotea katika injili ya Yesu. Ilikuwa wakati wa kurejesha Kanisa Lake! Baba wa Mbinguni alihitaji mtu awe nabii na asaidie kulirejesha duniani. Alimchagua mvulana mdogo aliyeitwa Joseph Smith.

Bible

Siku moja, Joseph alikuwa akisoma Biblia. Katika Yakobo 1:5, ilisema kwamba Baba wa Mbinguni atajibu maswali yetu wakati tunapouliza kwa imani. Joseph alikuwa na swali! Alijua kulikuwa na makanisa mengi ambayo yalifundisha kuhusu Yesu. Lakini alitaka kujua kama kulikuwa na moja kama lile Kanisa la Yesu katika Agano Jipya.

Joseph praying

Katika siku nzuri ya majira ya kuchipua karibia na Pasaka, Joseph alikwenda msituni karibu na nyumbani kwao. Alipiga magoti na kuanza kusali. Kisha Joseph akahisi hisia ya giza. Shetani alikuwa anajaribu kumvunja moyo. Lakini Joseph aliendelea kusali kwa uwezo wake wote.

First Vision

Kisha nuru nzuri ikashuka chini. Joseph aliwaona Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo. Hii inaitwa Ono la Kwanza. Walisema kwamba Kanisa la Yesu Kristo halikuwepo duniani. Lakini lingekuwapo karibuni. Urejesho ulikuwa unaanza!

Angel Moroni

Baba wa Mbinguni aliwatuma malaika kurejesha vipengele muhimu vya injili. Malaika Moroni alimpatia Joseph bamba za dhahabu ili tuweze kupata Kitabu cha Mormoni kutusaidia kujifunza kuhusu Yesu Kristo.

little girl being confirmed

Yohana Mbatizaji alirejesha Ukuhani wa Haruni ili tuweze kubatizwa. Petro, Yakobo, na Yohana walileta ukuhani wa Melkizedeki ili tuweze kupokea Roho Mtakatifu na kupata baraka wakati tunapougua.

family in front of the temple

Eliya alikuja ili tuweze kuunganishwa na familia zetu hekaluni.

family going to church

Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho lilianzishwa. Hii inamaanisha kwamba Kanisa la Yesu limerejea duniani! Vitu hivi vyote ni sehemu za Urejesho.

serving

Urejesho wa Injili ungali unaendelea leo hii. Manabii, mitume, wamisionari, na waumini wanashiriki habari njema ya Yesu Kristo kote ulimwenguni. Mahekalu yanajengwa katika nchi nyingi ili watu waweze kuunganishwa na familia zao milele. Na kanisa linawasaidia watu katika maeneo ambayo kuna njaa au maafa.

temple, family history, tithing

Kila mtu anaweza kufanya kitu kutoa msaada kwa Urejesho. Unaweza kusaidia kwa kujifunza kuhusu historia ya familia yako na kufanya ubatizo wa hekaluni. Unaweza kutoa zaka kujenga makanisa na mahekalu. Unaweza kutoa matoleo ya mfungo kuwasaidia watu wenye mahitaji. Unaweza kuwaelezea watu kuhusu Yesu Kristo.

boy taking the sacrament

Yesu Kristo alitupatia Kanisa Lake kutusaidia sisi kurudi kwa nyumbani kwetu mbinguni. Tunaweza kushiriki sakramenti na daima kukumbuka kile Alichofanya kwa niaba Yetu. Tunawezaje kuonesha upendo kwa wengine, kama Alivyofanya. Tunaweza kumsaidia kila mtu kujifunza kuhusu injili yake! ●

Vielelezo na Apryl Stott