2020
Kuboresha Uzoefu Wetu wa Hekaluni
Aprili 2020


Kuboresha Uzoefu Wetu wa Hekaluni

“Taji ya kito ya Urejesho ni hekalu takatifu. Ibada zake na maagano matakatifu ni ya msingi katika kuwaandaa watu walio tayari kumkaribisha Mwokozi katika Ujio Wake wa Pili.”1

Kwa wakati ufaao, Urais wa Kwanza umefanya marekebisho kwenye ibada za hekaluni na taratibu ili kuboresha uzoefu wa hekaluni kwa waumini na kuwasaidia wote wanaoingia kuhisi uhusiano wa karibu na Mungu katika mazingira haya matakatifu.

Kama sehemu ya uzoefu wa hekaluni, washiriki huvalia mavazi maalum yenye umuhimu wa kimafundisho na kiishara ambayo asili yake inapatikana katika ibada ya hekaluni katika Agano la Kale (ona Mambo ya Walawi 8 na Kutoka 28).

Marekebisho kadhaa yamefanywa kwa mavazi maalum ya ibada ya hekaluni. Marekebisho haya hayaashirii mabadiliko kwenye ishara za hekaluni au mafundisho lakini yamekusudiwa kufanya ibada ya hekaluni kuwa rahisi zaidi, ya kuliwaza, na ya kupatikana kwa urahisi kwa kuyafanya mavazi kuwa rahisi kuvaliwa, kuyatunza, na bei nafuu.

Baadhi ya marekebisho haya ni pamoja na:

  • Mtindo rahisi zaidi wa shela na joho.

  • Kuondoa plastiki iliyotiwa ndani ya kofia na tai kutoka kwenye kofia na shela.

  • Kutumia kitambaa cha kudumu zaidi ambacho kinatumika kwenye joho, kofia, na mshipi, ambacho kinavisadia kudumu kwa muda mrefu zaidi na kuvifanya rahisi kuvitunza.

Tunatumaini marekebisho haya yatasaidia kuboresha uzoefu huu mtakatifu kwa ajili yako unapofanya ibada ya hekaluni kuwa sehemu ya kawaida katika maisha yako.

Muhtasari

  1. Russell M. Nelson, “Maneno ya Kutamatisha,” Liahona, Nov. 2019, 120.