Njoo, Unifuate: Kitabu cha Mormoni
Inamaanisha Nini Kuwa na Jina la Kristo Kuandikwa Katika Mioyo Yetu?
Aprili 20–26 Mosia 4–6
Katika Kitabu cha Mormoni, watu wanaitwa kwa majina mengi—Wanefi, Walamani, na Waanti-Nefi-Lehi ni baadhi tu. Lakini Mfalme Benyamini alitaka watu wake waitwe kwa jina la juu, takatifu zaidi—jina la Yesu Kristo.
Hivi ndivyo tunavyoweza kudumisha jina la Mwokozi likiwa “limeandikwa daima mioyoni [mwetu]” (Mosia 5:12):
Fanya maagano kupitia Ubatizo
Wakati wa ubatizo, tunaagana na Mungu kujichukulia juu yetu jina la Kristo. Unafikiri hiyo ina maana gani? (Ona Mosia 18:8–9.)
Shiriki Sakramenti
Tumeamriwa kushiriki sakramenti kwa ustahiki kila wiki. Wakati wa sakramenti, tunafanya upya agano letu la kujichukulia juu yetu jina la Yesu Kristo (ona Moroni 4:3).
Tenda kama Mfuasi wa Kristo
Maagano yetu yanatutaka kutii amri. Vitendo vyetu vinapaswa kuonesha nia yetu ya kumfuata Yesu Kristo na kuwa kama Yeye. Kwa kufanya hivyo, tunaweza kuendelea kuitwa kwa jina Lake. Hivi ndivyo tunavyoweza kudumisha jina la Kristo likiwa limeandikwa daima mioyoni mwetu (ona Mosia 5:12).