2020
Baraka Pekee Ndiyo Niliweza Kutoa
Aprili 2020


Baraka Pekee Ndiyo Niliweza Kutoa

Jonathan Mafra Sena de Santana

Santa Catarina, Brazil

Picha
father giving daughter a blessing

Kielelezo na Allen Garns

Nilimaliza chuo cha mafunzo ya sheria karibu na wakati ambapo binti yangu alikuwa akisherehekea mwaka wa kwanza wa kuzaliwa. Mimi na mke wangu tulikuwa tunasubiri kusherehekea kuhitimu kwangu, siku ya kuzaliwa ya binti yetu, na nafasi mpya ambazo tungepata, lakini hakuna kilichofanyika kulingana na mipango yetu.

Nilijikuta bila kazi muda mfupi baada ya kumaliza shahada yangu na nilikuwa na wakati mgumu kupata kazi. Mara, changamoto za kiuchumi zikaja. Kuwa na sherehe ndogo ya siku ya kuzaliwa ingekuwa vigumu.

Baada ya mazungumzo mengi na mke wangu, tulikubali hali yetu. Haikuwa rahisi kwangu kama baba kutokuwa na uwezo wa kununua hata zawadi ndogo kwa ajili ya binti yangu na kuona mke wangu mpendwa akihisi kukata tamaa.

Sikuelewa kilichokuwa kikifanyika. Nilisali na kumwomba Baba wa Mbinguni anisaidie kuelewa kile ambacho Alitarajia nifanye. Ghafla, kana kwamba sauti ilinena akilini mwangu, nilisikia maneno yafuatayo: “Unamiliki kitu chenye thamani kuliko mali yote iliyopo humu duniani. Unamiliki ukuhani. Ni baraka ipi bora unaweza kumpa binti yako kuliko baraka ya ukuhani?”

Machozi yalijaa machoni mwangu nilipofikiria kuhusu maana ya ukuhani kwangu mimi. Moyo wangu ulijawa na shukrani wakati nilipofikiria kwamba ukuhani ni nguvu ambayo inaweza kuileta pamoja familia yangu milele.

Nilishiriki hisia zangu pamoja na mke wangu. Nilimwambia kwamba kumpatia baraka ya ukuhani binti yangu ilikuwa kitu pekee ambacho ningeweza kutoa. Sote tuliamua kwamba hilo lingeleta furaha na amani kwake, na hilo lingetosha.

Siku ya kuzaliwa kwa binti yetu, marafiki, jamaa, na majirani walileta keki na mapambo ya kawaida. Tulikuwa na shukrani kusherehekea siku hii maalum pamoja na wale tunaowapenda. Usiku huo, niliweka mikono yangu juu ya kichwa cha binti yangu na kumpa baraka. Nilimbariki kwa kila kitu Roho wa Bwana alichoniongoza kusema.

Bado tunapitia kipindi cha mabadiliko na changamoto kuhusu kukosa kazi na fedha. Lakini hata katikati ya huzuni na kukata tamaa, amani na faraja huja kwetu kupitia Mwokozi wetu, Yesu Kristo. Sina wasiwasi kwamba kuwa muumini wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho na kufikia nguvu za ukuhani ni baraka. Ilikuwa kitu pekee ambacho ningeweza kumpa binti yangu katika siku yake ya kuzaliwa, na hiyo ilitosha.

Chapisha