2020
Kuhudumu kupitia Mkutano Mkuu
Aprili 2020


Kanuni za Kuhudumu

Kuhudumu kupitia Mkutano Mkuu

Pamoja na dondoo zote za kuinua, desturi za familia, na mafundisho kutoka kwa watumishi wa Bwana, mkutano mkuu unatupatia njia nyingi za kuhudumu—kabla, wakati wa, na baada ya wikiendi ya mkutano mkuu!

scenes from general conference

Kama walimu wa darasa la matayarisho ya misheni, Susie na Tom Mullen kawaida wao huwapa washiriki wa darasa lao changamoto ya kumwalika mtu fulani kutazama mkutano mkuu pamoja nao.

“Kumwalika mtu kufanya jambo fulani ni sehemu muhimu ya kazi ya umisionari, na inatumika kwenye kuhudumu pia,” anasema. “Wanafunzi wetu hutoa ripoti mara kwa mara kuhusu jinsi ilivyofanyika vyema kwao na pia mtu ambaye walimualika.”

Hapa ni njia chache ambazo wanafunzi wao waliripoti kuhusu kufikia:

  • “Sisi humhudumia rafiki ambaye ana shida fulani anazopambana nazo. Tulimualika asikilize mkutano mkuu kwa ajili ya majibu. Wakati tulipomtembelea baada ya mkutano mkuu, alituelezea kwamba alisikia mawazo mengi ambayo yangemsaidia.”

  • “Tulifanya sherehe ya mkutano mkuu na kila mtu alileta asusa za kushiriki. Ilikuwa furaha kubwa kwamba tuliamua kufanya hivyo tena.”

  • “Nlimualika rafiki atazame mkutano mkuu pamoja nami. Tulipokuwa tukizungumza kuhusu mkutano mkuu, tuliamua kusafiri kwa gari hadi kwenye jumba la mikutano kuona kama tungeweza kuutazama kutokea pale. Tuliweza, na ilikuwa uzoefu mzuri zaidi kuwa pale!”

Jinsi akina Mullen na wanafunzi wao walivyojifunza, kuna njia nyingi za kuhudumu kupitia mkutano mkuu. Ni njia nzuri ya kushiriki dondoo za kuinua, desturi za familia, mijadala ya maana, na mafundisho ya watumishi wa Bwana!

Alika Wengine Nyumbani Kwako.

“Mwokozi aliwaamuru wafuasi Wake ‘mpendane, kama nilivyowapenda ninyi’ (Yohana 13:34). Kwa hivyo tunaangalia jinsi Alivyotupenda. … Kama tutamchukua Yeye kuwa mfano wetu, ni sharti siku zote tujaribu kumjumuisha kila mtu.” —Rais Dallin H. Oaks1

Miaka mingi iliyopita mwalimu wetu wa nyumbani Mike aligundua kwamba mimi na watoto wangu watatu tulikuwa na kompyuta ndogo ya kutazama mkutano mkuu. Mara moja alitualika kwenda nyumbani kwake kutazama pamoja naye na mkewe, Jackie, akisisitiza kwamba tungefurahia wenza wao. Watoto wangu walifurahia kutazama mkutano kwenye TV ya kweli; nilifurahia pakubwa kupata msaada huo; na tulifurahia wakati wetu pamoja.

Baada ya hapo, kutazama mkutano mkuu pamoja ilikuwa desturi. Hata baada ya kupata TV yetu, kwa furaha bado tulienda kwa Mike na Jackie na mito yetu, madaftari, na asusa kwa ajili ya mkutano mkuu. Kusikia maneno ya manabii pamoja iliufanya kuwa maalum. Tulikuwa kama familia. Mike na Jackie walikuja kuwa baadhi ya rafiki zangu wazuri zaidi na mababu wa pili kwa watoto wangu. Upendo na urafiki wao umekuwa baraka ya ajabu kwa familia yangu. Nina shukrani kwa ajili ya utayari wao kufungua nyumba yao na mioyo yao kwetu.

Suzanne Erd, California, Marekani

Kanuni za Kuzingatia

“Tambua”

Mwokozi kwa upendo alitumia muda kuona mahitaji ya wengine kisha akashughulikia mahitaji hayo (ona Mathayo 9:35–36; Yohana 6:5; 19:26–27). Tunaweza kufanya vivyo hivyo.

“Alika mara moja”

Baada ya kutambua mahitaji ya wale tunaowahudumia, hatua inayofuata ni kutenda.“Kusikia maneno ya manabii”

Ni sharti “kukutana pamoja mara kwa mara” (Moroni 6:5) kujifunza pamoja, kukua pamoja, na kuzungumza kuhusu vitu vya kiroho ambavyo ni vya muhimu zaidi kwa nafsi zetu.

“Njoo, usikie sauti ya nabii, na usikie neno la Mungu”2 unaweza kuwa mwaliko muhimu zaidi tunaowapa wale tunaowahudumia.

“Upendo na urafiki”

Ili kuwasaidia na kuwashawishi wengine kwa kweli, ni lazima tujenge mahusiano ya huruma na “upendo usio unafiki” (ona Mafundisho na Maagano 121:41).

looking at a tablet

Shiriki kwenye mtandao

“Mitandao ya kijamii ni vifaa vya kimataifa ambavyo vinaweza kibinafsi na kwa njia chanya kuathiri idadi kubwa ya watu binafsi na familia. Ninaamini wakati umefika kwetu kama wafuasi wa Kristo kutumia zana hizi zenye ushawishi kwa usahihi na kwa weledi zaidi kushuhudia juu ya Mungu Baba wa Milele, mpango Wake wa furaha kwa watoto Wake, na Mwanawe, Yesu Kristo, kama Mwokozi wa ulimwengu.” —Mzee David A. Bednar3

Wavuti inaturuhusu kushiriki injili pamoja na ulimwengu mzima. Ninalipenda hilo! Hii inajumuuisha sehemu ya mkutano mkuu ambapo mimi hushiriki shughuli chache kwa ajili ya mkutano mkuu, lakini sana sana mimi hujaribu kuwasaidia wengine kubuni mjadala kutoka kwenye hotuba za mkutano mkuu. Kuona maswali kutoka kwa wengine kawaida kunaweza kutusaidia kuona vitu kwa mtazamo mpya na inaweza kuwa ubao wa kutupia maswali yetu makuu ya mjadala.

Nimegundua kwamba unapotumia maswali kujadili hotuba za mkutano mkuu pamoja na familia unazozihudumia, hilo linakusaidia kuona nguvu yao na vile vile mahitaji yao. Mojawapo ya maswali ninayopenda kuuliza ni, Unahisi nini ilikuwa dhamira kutoka kwenye kikao cha hivi karibuni cha mkutano mkuu?

Jibu karibu kila wakati linakuwezesha kuona kile kinachoendelea katika maisha yao na kile ambacho ni muhimu kwao. Inatoa nafasi kwako kuwa kaka au dada bora mhudumiaji kwa sababu unapata nafasi ya kuwaona kwa uwazi zaidi.

Camille Gillham, Colorado, Marekani

Kanuni za Kuzingatia

“Shiriki injili”

Tumeweka agano “kusimama kama mashahidi wa Mungu nyakati zote, na katika vitu vyote na katika mahali popote” (Mosia 18:9).

“Buni mjadala”

Jumbe za mkutano mkuu zinaweza kutia msukumo wa mazungumzo, mazuri, yanayofaa, na yanayoongozwa kiroho. Na mijadala ya aina hii inaweza kuimarisha mahusiano, kusaidia ushuhuda kukua, na kukuletea furaha! (ona Mafundisho na Maagano 50:22).

“Tumia maswali”

“Maswali mazuri yatakusaidia kuelewa mapendeleo, wasiwasi, au maswali ambayo wengine wanayo. Yanaweza kuboresha kufundisha kwako, kualika Roho, na kuwasaidia watu kujifunza.”4

Muhtasari

  1. Dallin H. Oaks, “Upendo na Sheria” (video), mormonandgay.ChurchofJesusChrist.org.

  2. “Come, Listen to a Prophet’s Voice,” Nyimbo za Kanisa, na. 21.

  3. David A. Bednar, “Kujaza Dunia kupitia Mitandao ya Kijamii,” Liahona, Ago. 2015, 50.

  4. Hubiri Injili Yangu: Mwongozo wa Huduma ya Umisionari (2004), 185.