Njoo, Unifuate: Kitabu cha Mormoni
Je, tunawezaje kupata nguvu ya uponyaji ya Kristo?
(Septemba 28–Octoba 11)
Katika huduma ya Yesu Kristo kwa Wanefi, Yeye alionyesha upendo mkubwa na nguvu Yake ya uponyaji kwa wote waliomwendea. Je, tunaweza kujifunza nini kutoka kwenye tukio la Wanefi na Mwokozi?
Majaribu ya Wanefi
Miongo kadhaa kabla ya kuwasili kwa Yesu ilikuwa ya misukosuko. Wanefi walivumilia:
-
Raia kuasi serikali(ona 3 Nefi 7:1-4).
-
Uovu na machukizo (ona 3 Nefi 2:3; 7:7.
-
Ubaguzi wa kitabaka (ona 3 Nefi 6:10 - 14).
-
Mateso ya kidini (ona 3 Nefi 1:9.
-
Vita (ona 3 Nefi 2:17).
-
Majanga ya asili wakati wa siku tatu za giza (ona 3 Nefi 8).
Huduma ya Kristo kwa Wanefi
Wakati Mwokozi alipowatokea Wanefi, Yeye aliwaalika wote waliokuwa ”wakiteseka kwa njia yoyote” (3 Nefi 17:7) kuja mbele na waponywe. Mwaliko Wake ulienda zaidi kupita majaribu ya wakati huo ya Wanefi. Ulihusu vidonda vilivyoonekana na visivyoonekana ambavyo Wanefi walibeba katika maisha yao yote. Yesu Kristo alimponya “kila mmoja” (3 Nefi 17:9) na aliwahudumia “mmoja mmoja” (3 Nefi 17:21).