Kuzuia Unyanyasaji
Katika uhusiano mzuri, watu huomba radhi kwa maneno na vitendo vyao visivyofaa na hutegemea nguvu za upatanisho za Mwokozi wetu ili kuwasaidia kujiboresha na kutubu. Lakini katika hali mbaya, watu wanaendelea kuwatendea vibaya wengine, na uhusiano huo unaweza kuwa unyanyasaji.
“[Unyanyasaji na makosa] mengine ya aina hiyo hayana nafasi katika ufalme wa Mungu,” alifundisha Rais Russell M. Nelson (“Hazina za Kiroho,” mkutano mkuu wa Oktoba 2019). Makala kadhaa za jarida la Kanisa mwezi huu zitatusaidia kutambua na kuongelea unyanyasaji.
-
Katika makala yangu kwenye ukurasa wa 18, naongelea kuhusu tabia za unyanyasaji na kutambua vyanzo fulani vya kukusaidia wewe au watu unaowajua kutambua na kuponywa kutokana na uhusiano wa unyanyasaji.
-
Kwenye ukurasa wa 58 msichana anaelezea uzoefu wake wa kunyanyaswa kingono akiwa mtoto na jinsi alivyoweza kupata ujasiri na nguvu ya kuongea na kutafuta msaada kutoka kwa watu wazima wanaoaminika na kwa Mwokozi.
-
Katika jarida la Rafiki la mwezi huu kwenye ukurasa wa 12, unaweza kutafuta shughuli ya kuandika ili kusaidia kujadili “kusema hapana” pamoja na watoto wako. Fikiria kutumia shughuli hii kama msingi wa somo la jioni ya nyumbani juu ya kuzuia unyanyasaji.
-
Unyanyasaji wa kihisia unaweza kuwa hatarishi sawa na aina zingine za unyanyasaji. Soma Kutambua Unyanyasaji wa kihisia katika toleo la kidijitali la makala hii ili kujifunza ishara tano za onyo na jinsi ya kupata msaada.
Ikiwa umeumizwa, unaweza kumgeukia Mungu kwa ajili ya mwongozo na uponyaji na pia utafute msaada kutoka kwa watu unao waamini. Bwana anaelewa kile tunachohisi, na atatuongoza kwa usalama na furaha tunapomgeukia Yeye.
Hebu sote na tuhisi upendo wa Mungu na kumfikia Yeye kila siku.
Jason Whiting, PhD
Chuo Kikuu cha Brigham Young Shule ya Maisha ya Familia