2020
Sakiusa na Salote Maiwiriwiri
Oktoba 2020


Taswira za Imani

Sakiusa na Salote Maiwiriwiri

Suva, Fiji

Sakiusa and Salote

Sikuweza kuamini amani na furaha niliyoipata katika nyumba ya Maiwiriwiri. Licha ya kufiwa na watoto wao wawili, wanaishi maisha yao kwa furaha na kusudi kila siku.

Leslie Nilsson, Mpiga picha

Salote:

Miaka miwili baada ya mwana wetu Esa kufariki kwa saratani ya mapafu, binti yetu Esalynn alifariki kwa ugonjwa wa uti wa mgongo. Hekaluni, nilihisi nguvu kubwa ya kuongea na mmisionari mkubwa wa kike ambaye pia alipoteza watoto wawili miaka ya nyuma. Aliniambia, “Kama utapafanya nyumbani kwako mahali patakatifu, unaweza kuhisi uwepo wa watoto wako huko.”

Hilo limekuwa lengo letu. Kila kitu tunachofanya ni kuzifanya nyumba zetu kuwa mahali patakatifu. Tunataka kuhisi ukaribu wao.

Hatujui jinsi ya kuwalea watoto nje ya pazia. Lakini tukifanya bidii kuishi kwa haki, tunaamini watahisi juhudi zetu. Katika ibada zetu za familia, tunawakaribisha Esa na Esalynn kwa jina.

Katika nyumba yetu, hata wakati ambao hatukubaliani, tunajaribu kuyatatua haraka. Tunataka nyumba yetu ibaki mahali patakatifu kadiri iwezekanavyo. Kama tumefanya hivyo, sote tumehisi tumaini na uponyaji na upendo.

Sakiusa:

Uzoefu wa kuwapoteza Esa na Esalynn mwishowe umeileta familia yetu pamoja. Tunashauriana pamoja na watoto wetu wengine. Tunahudhuria hekaluni kama familia. Tunaishi maisha yetu kawaida kadiri iwezekanavyo na tunachagua shukrani kila siku. Tunapoongea juu ya nini maana ya kuunganishwa kama familia katika hekalu, kuunganishwa huko kunakuwa hai ndani yetu. Na kupitia haya yote, sisi tunahisi uwepo wa watoto wetu.

Moja ya mambo ya kwanza tuliyoyafanya ili kuifanya nyumba yetu kuwa takatifu zaidi ni kusoma Kitabu cha Mormoni kila siku. Kwanza, tulishiriki hadithi za Kitabu cha Mormoni chenye picha kwa ajili ya watoto wetu wadogo. Kisha tukaongeza video. Sasa tunasoma zaidi kutoka kwenye Kitabu cha Mormoni. Ninaweza kushuhudia juu ya nguvu ya Kitabu cha Mormoni.

Pia ninaweza kushuhudia nguvu iliyoko katika mpango wa wokovu. Wakati tulipopanga mazishi ya Esa na Esalynn, tuliamua kinyume na mazishi ya kawaida katika utamaduni wa Fiji. Badala yake, mke wangu na mimi ndio tulikuwa waongeaji pekee, na tuliongea kuhusu mpango wa wokovu. Wanafamilia wetu wengi wamejiunga na Kanisa baada ya kusikia ukweli huu kutokana na huduma za mazishi.

Sakiusa in the kitchen

Sakiusa anaifundisha familia yake kwamba hakuna kurudi nyuma katika maisha, ni mbele tu. “Kila siku tunafanywa safi zaidi,” anasema. Wanaishi maisha yao kawaida kadiri iwezekanavyo na huzingatia shukrani.

Salote with a little girl

Salote anapata furaha kubwa katika kutumia muda na watoto wake na katika kuwafundisha injili.

Little girl holding up photo

Familia ya Maiwiriwiri ina ushuhuda imara wa kuunganishwa katika hekalu. Wanaweka ukweli huu karibu na mioyo yao wakiwa wanawakumbuka Esa na Esalynn.

Maiwiriwiri family smiling boys

Wanapozingatia kuishi maisha ya kawaida na kusonga mbele, familia ya Maiwiriwiri hupata shukrani kwa baraka zao kila siku. “Tunashukuru kwa kile tulicho nacho,” Sakiusa anasema.