Njoo, Unifuate: Kitabu cha Mormoni
Je, ni kwa jinsi gani sisi tunashiriki katika “kazi ya ajabu” ya Bwana?
(Oktoba 12-18)
Miongoni mwa mambo mengi ambayo Mwokozi aliwafundisha Wanefi, aliwafundisha juu ya kukusanyika kwa Israeli na aliwaamuru kusoma maandiko na kuweka kumbukumbu zao wenyewe. Tunawezaje kufuata mafundisho haya leo?
Jiunge kwenye Kazi
Yesu Kristo alitoa unabii juu ya “kazi ya ajabu” katika siku za mwisho (ona 3 Nefi 21:9). Kazi hiyo ni kukusanywa kwa Israeli? Rais Russell M. Nelson ameita hili “jambo la muhimu sana linalofanyika duniani leo” na akasema, “Kama ukichagua, ikiwa unataka, unaweza kuwa sehemu kubwa ya hilo.”1
-
Je, wewe na familia yako mnawezaje kujifunza zaidi juu ya na kushiriki katika kukusanywa kwa Israeli?
Pekua Manabii
Mwokozi aliwaamuru Wanefi “pekua manabii” (3 Nefi 23:5). Sisi tunayo fursa ya kumsikia nabii aliye hai na viongozi wengine wa Kanisa wakiongea katika mkutano mkuu.
-
Je, unaweza kufanya nini ili kupata mengi kutoka kwenye mkutano mkuu?
-
Je, “kupekua manabii” kunatusaidiaje katika kuikusanya Israeli?
Weka Kumbukumbu
Yesu aliwaamuru wanafunzi Wake Wanefi kuweka kumbukumbu ya mafundisho Yake na unabii wa Samweli Mlamani (ona 3 Nefi 23:4, 6–13). Vivyo hivyo, tunaweza kurekodi uzoefu wetu wa maisha ili kutusaidia na kufundisha wengine.
-
Kuna matukio ya zamani ya kiroho ambayo haujayarekodi?
-
Je, unawezaje kurekodi mambo ambayo Mungu anakufundisha wewe?