2020
Ni kwa jinsi gani ninaweza kushinda hisia za upweke?
Oktoba 2020


Maswali & Majibu

Ni kwa jinsi gani ninaweza kushinda hisia za upweke?

girl with her head down

Picha na Kay Lynn Hodges

Kuza Vipaji Vyako

Ninashinda hisia zangu za upweke kwa kukuza vipaji vyangu, iwe ni kifaa cha muziki, jambo nilipendalo, n.k. Hii husaidia kukuondoa kutoka kwenye hisia zako za upweke, na mara nyingi zitaondoka kabisa. Hii pia itakuelekeza kuwatafuta wengine ambao wanashiriki maslahi yako.

Steven H., miaka 12, New Mexico, Marekani

Tafuta Nuru

Natafuta msaada, kutiwa moyo, na upendo wa Baba wa Mbinguni na Roho Mtakatifu kunipa amani, matumaini, na nguvu wakati wa kutafakari, kuomba, na kusoma maandiko. Kama inavyonena katika 3 Nefi 11:11, Yesu Kristo ni “nuru na uzima wa ulimwengu.” Alikuja kuondoa giza lote.

Andrea B., miaka 18, Zulia, Venezuela

Wafikie Marafiki na Familia

Wakati ninahisi kuwa peke yangu, napenda kuwafikia marafiki na familia yangu; kwa kweli inanifanya nifurahi. Ninaangalia baraka maishani mwangu na namshukuru Baba wa Mbinguni kwa kiasi ambacho tayari amenipa!

Talli N., miaka 16, Oregon, Marekani

Kumbuka Mpango wa Mungu

Jua kuwa kupitia mpango wa Mungu, sisi ni kila kitu lakini wapweke. Roho Mtakatifu yupo pamoja nasi daima, na Mungu anajua yale tunayosumbuka nayo. Bwana alipitia kila jaribu na mapambano unayopitia. Mojawapo ya mambo muhimu ambayo tunahisi duniani ni furaha, lakini hatuwezi kuwa na furaha bila huzuni (ona 2 Nefi 2:11). Omba kwa Mungu na muombe msaada; Hawezi kutuangusha sisi.

Brock S., miaka 17, Utah, Marekani

Mtumaini Bwana

Kuondoka nyumbani kuja Brazil kwa ajili ya misheni ilikuwa vigumu. Sikuweza hata kuongea lugha ya huku! Lakini nimejifunza kuwa ikiwa Roho wa Bwana yuko pamoja nawe, hautahisi upweke kamwe. Anakujua na daima atakusaidia. Mwamini Yeye!

Mzee Joseph Tolen, miaka 20, Misheni ya Brazil Campinas