Vijana
Wakati niliposimikwa ili kuhudumu katika misheni ya California San Bernardino kama mmisionari, familia yangu ilikuwa pale pamoja nami. Picha hii ni yangu mimi nikimkumbatia mmoja wa kaka zangu baada ya kusimikwa. Imekuwa ni safari hadi kufika hapa, lakini nashukuru sana kwa mabadiliko ambayo nimeyaona kwangu na katika familia yangu.
Mwaka wangu wa pili-kwenda-wa mwisho wa shule ya upili ya juu, nilipata ajali mbaya ya gari. Kabla ya hapo sikuwa nafanya mambo niliyopaswa kufanya. Lakini baada ya ajali, mtazamo wangu kweli ulibadilika. Maisha yangu yangewweza kutwaliwa wakati huo na pale, na sikutaka yaishie kama hivyo. Askofu wangu alinisaidia kuniweka kwenye njia sahihi: kusoma Kitabu cha Mormoni kila siku na kujiandaa kuhudumu misheni.
Mbio za miguu ndio mchezo wangu, shauku yangu. Baada ya kuvunjika, nilikuwa nje kwa msimu, na nilijiuliza hata nilikuwa nimeacha nini. Lakini nilimgeukia Bwana, na nilipofanya hivyo, nikawa na msimu mzuri mwaka uliofuata. Bado kulikuwa na mapambano, lakini kilichobadilika badala ya kuifanya kwa ajili yangu, niliifanya kwa ajili ya Bwana.
Ile kuona tu ni baraka ngapi zinaweza kuja kutokana na utimilifu wa injili ndio kitu killicho nibadilisha. Kupata furaha na shangwe hiyo yote, ninataka kueneza kuzunguka ulimwengu. Natamani watu wawe na furaha ambayo mimi ninayo kila siku kwa sababu ya injili. Na hii ndiyo sababu ninahudumu misheni: ili kusaidia “kuleta kutokufa na uzima wa milele wa mwanadamu” (Musa 1:39).
Garret W., 18, Carolina Kaskazini, Marekani