2020
Unaweza Kupata Uhuru
Oktoba 2020


Vijana Wakubwa

Unaweza Kupata Uhuru

friends smiling

Je, wewe au mtu unayempenda ameshikwa kwenye mzunguko wa kufanya makosa, kutubu, kutenda tena, na kufanya tena makosa? Vijana wengi wakubwa wazuri ambao nilifanya nao kazi wakati nikihudumu kama askofu wa kata ya vijana wakubwa waseja walikuwa wameshikwa kwenye mzunguko huo huo. Lakini wengi pia walipata uhuru kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo. Ujumbe juu ya uraibu katika sehemu ya mwezi huu unatoa msaada wa utambuzi ili kupata uhuru—kwa ajili yako mwenyewe na kwa ajili ya wengine.

Jambo muhimu zaidi ambalo tunapaswa kukumbuka ni kwamba sisi sote ni watoto wapendwa wa Baba wa Mbinguni. Mzee Dieter F. Uchtdorf alifundisha, “[Mungu] hangoji kukupenda hadi wewe ushinde mapungufu yako na tabia mbaya. Anakupenda leo kwa ufahamu kamili wa mapambano yako. … Anajua kuhusu majuto yako kwa ajili ya nyakati unapokuwa umepungukiwa ama kushindwa. Na bado Anakupenda” (“Kuishi Injili kwa Furaha,” Liahona, Nov. 2014, 123; msisitizo umeongezwa).

Kwa upande mwingine, Shetani atajaribu kukushawishi kwamba wewe ni zaidi ya na umeondolewa kutoka kwenye upendo wa Baba wa Mbinguni na nguvu ya Mwokozi ya kukubadilisha na kukusafisha. Shetani atajaribu kukuweka kwenye kizingia cha maji na kujichukia mwenyewe, lakini usiamini uwongo wake.

Badala yake, mgeukie Baba wa Mbinguni. Usiogope kusema ukweli kwa askofu wako au rais wa tawi na wengine wanaokupenda. Unaposoma hadithi za matumaini kutoka kwa vijana wakubwa wengine ambao wameathiriwa na uraibu fanya kulingana na ushawishi unaopokea. Kuwa na uvumilivu kwako wewe mwenyewe, kumbuka asili yako ya kiungu, chukua siku moja baada ya nyingine, na uamini katika uweza wa uponyaji wa Yesu Kristo. Yeye na nyenzo nyingine nyingi zitatusaidia kufanikiwa kupata uhuru tunaotamani. Usikate tamaa kamwe.

Rafiki yako,

Richard Ostler