Kutafuta Amani
“Tafadhali nisaidie nisijione mpweke.”
Molly alijizuia kutolia alipokuwa anamuaga dada yake, Macy. “Ninakupenda!” Molly alisema. Molly alimpa Macy kumbatio kubwa.
“Nitakuona ndani ya miezi michache,” Macy alisema. Macy alikuwa anaondoka nyumbani sasa kuelekea chuoni. Mmoja wa kaka za Molly tayari alikuwa yuko chuoni. Kaka yake mwingine alikuwa anahudumu misheni. Molly angewakumbuka wote sana!
Mama aliuminya mkono wa Molly. Walimuangalia Macy akiondoka. “Tutamkumbuka,” Mama alisema. Mama alikuwa na machozi machoni mwake.
Molly alitembea kuingia ndani ya nyumba. Aliingia ndani mwa chumba kitupu cha Macy na kufunga mlango. Kisha alikaa juu ya kitanda cha Macy na kuanza kulia.
Mtu aligonga mlango. Mama na Baba waliingia. Walimkumbatia Molly. Wote walikaa juu ya kitanda cha Macy mpaka machozi ya Molly yalipokauka.
“Najua una huzuni juu ya kuondoka kwa Macy,” Baba alisema. “Kwa nini tusifanye sala ya familia? Tunaweza kumwomba Baba wa Mbinguni ili atusaidie tujisikie vizuri zaidi. Molly, unaweza kusali tafadhali?”
“SAWA.” Molly aliinamisha kichwa chake. “Baba wa Mbinguni, tunakushukuru kwa ajili ya kila mmoja ndani ya familia yetu—kwa ajili ya Will, Parker, Macy, mimi mwenyewe, na Mama na Baba. Tunakushukuru kwamba tunaweza kuwa familia milele. Tafadhali tusaidie tuhisi faraja. Na nisaidie mimi nisijihisi mpweke.”
Molly alikumbuka kuongea na Macy wakati wa kulala. Lakini alijua Baba wa Mbinguni amesikia maombi yake. Alijua Yeye angemsaidia ili ahisi vizuri zaidi.
Asubuhi iliyofuata, nyumbani kwao na Molly palikuwa kimya sana! Alikumbuka kucheka pamoja na Macy walipokuwa wakijiandaa kwa ajili ya shule. Alikumbuka kupata kifungua kinywa pamoja na kuongea. Wakati mwingine Macy alimwambia kuhusu kile anachojifunza katika darasa la seminari. Molly daima alijisikia mwenye amani walipokuwa wakiongelea kuhusu injili.
Hivyo ndivyo ilivyokuwa! Molly alipata wazo!
Molly alijiandaa kwa ajili ya shule. Kisha akamwona Mama.
“Mambo, kipenzi.” Mama alimkumbatia Molly. “Uko tayari kwa ajili ya shule?”
“Tunaweza kusoma hotuba moja ya mkutano mkuu pamoja kabla sijaondoka?” Molly aliuliza. “Nadhani itanisaidia nihisi vizuri zaidi.”
Mama alitabasamu. “Hilo ni wazo zuri sana.”
Walipokezana kusoma hotuba hiyo ya mkutano mkuu kuhusu faraja. Molly alipenda kutumia muda pamoja na mama yake. Ilionekana vyema kusoma hotuba hiyo pamoja naye.
Walipomaliza, Molly alitabasamu. “Na tufanye hili tena!”
Bado anawakumbuka Macy, Will na Parker. Lakini alihisi kupungua kidogo kwa upweke. Ombi lake lilijibiwa! Angeweza kutumia muda pamoja na mama na baba yake. Na maneno ya manabii yangemsaidia Molly kupata amani.