2022
Kutana na Alice kutoka Fiji
Machi/Aprili 2022


Mikono ya Usaidizi Ulimwenguni Kote

Kutana na Alice kutoka Fiji

Kutana na watoto wa Msingi wakiwasaidia wengine, kama Yesu alivyofanya.

Picha
photo of girl holding sign about free clothes

Yote kuhusu Alice

Picha
picture of Alice painting

Umri: miaka 10

Kutoka: Alizaliwa China na sasa anaishi Fiji

Lugha: Kichina and Kiingereza

Malengo na ndoto: 1) Kuwa mpaka rangi. 2) Kujua Kiingereza vyema kwa kusoma kuhusu Yesu.

Familia: Baba, Mama, dada na kaka

Mikono ya Usaidizi ya Alice

Picha
Alice and her family handing out clothes

Mama wa Alice ni daktari na baba yake anawafundisha watu katika mambo ya huduma ya kwanza. Alice na familia yake walianzisha timu ya kujitolea ya vijana ili kuwasaidia watu katika eneo lao.

Kwanza, wazazi wake waliwafundisha zaidi ya vijana 100 na wazazi wao katika mambo ya huduma ya kwanza. Alice alisaidia pia. Kisha timu ilikusanya aina zaidi ya 3,000 za nguo za kuvaa kwa ajili ya watu wenye shida. Pia walikusanya viatu vingi.

Polisi wa eneo hilo walipendezwa na kazi yao. Polisi waliipa timu ile meza hapo sokoni ili iwasaidie kutenda kazi njema kwa wingi.

“Sisi tunamwamini Mungu,” Alice anasema. “Kwa hiyo tunamhudumia kila mtu!” ●

Mambo Ayapendayo Alice

Picha
pictures of Alice’s favorites

Mahali: Ufukweni

Hadithi kuhusu Yesu: Wakati mwanamke katika umati alipogusa vazi Lake na akaponywa

Wimbo wa msingi: “I Want to Be a Missionary Now” (Kitabu cha Nyimbo cha Watoto, 168)

Chakula: Tambi

Rangi: Zambarau

Somo shuleni: Hisabati

Vielelezo na Anthony Lewis

Chapisha