Hadithi za Maandiko
Yusufu Anajiandaa kwa ajili ya Nyakati Ngumu
Unaweza kusoma hadithi hii katika Mwanzo 41.
Yusufu alikuwa Nabii. Aliishi Misri. Usiku mmoja Farao, mfalme wa Misri, alipata ndoto ya ajabu. Alimwuliza Yusufu maana ya ndoto hiyo.
Mungu alimsaidia Yusufu kuelewa ndoto hiyo. Kwa miaka saba, watu watakuwa na wingi wa chakula. Kisha kwa miaka saba, hawatakuwa na chakula cha kutosha. Yusufu alimwambia Farao.
Yusufu alisema walipaswa kuweka akiba ya chakula sasa. Ndipo wangekuwa tayari kwa ajili ya nyakati ngumu. Farao alimpa Yusufu jukumu la kuhifadhi hicho chakula. Yusufu alifanya kazi kwa bidii.
Wakati miaka saba ya njaa ilipokuja, watu walikuwa na chakula cha kutosha. Hata wakawa na ziada ya kuwapa wengine.
Ninaweza kujiandaa sasa. Kwa msaada wa Mungu, ninaweza kuvuka nyakati ngumu!