2022
Musa na Mana
Machi/Aprili 2022


Hadithi za Maandiko

Musa na Mana

Unaweza kusoma hadithi hii katika Kutoka 16.

Picha
Moses with lots of people walking behind him

Musa alikuwa nabii. Aliwaongoza watu wa Mungu kuelekea nchi ya ahadi. Walitembea kwa siku nyingi.

Picha
girl and boy holding food in hands

Watu walikuwa na njaa. Hawakuwa na chakula. Hivyo Mungu aliwatumia chakula kutoka mbinguni. Kiliitwa mana.

Picha
mom and son gathering food in bowl

Kila asubuhi, watu walikusanya mana ili wale. Lakini mana isingefaa kama ingekaa zaidi ya usiku mmoja. Ilibidi wakusanye zaidi siku iliyofuatia.

Picha
Jesus with young children

Mana hutukumbusha sisi kuhusu Yesu Kristo. Mungu alituma mana ili kuwaokoa watu. Pia alimtuma Yesu duniani ili kutuokoa sisi. Tunamhitaji Yesu kila siku, kama tunavyohitaji chakula kila siku.

Picha
boy showing picture of Jesus to little sister

Nitamfuata Yesu. Yeye atanipa nguvu na kunisaidia kuhisi upendo Wake kila siku.

Picha
coloring page of Jesus with children

Vielelezo na Apryl Stott

Chapisha