2022
Halo kutoka Fiji!
Machi/Aprili 2022


Halo kutoka Fiji!

Ungana na Margo na Paolo wanaposafiri kuzunguka ulimwengu ili kujifunza kuhusu watoto wa Baba wa Mbinguni.

Fiji ni nchi ya kisiwa huko Bahari ya Pasifiki ya Kusini. Ina visiwa zaidi ya 330!

Msaidizi Mwenye Furaha

Picha
boy sweeping at church building

Mvulana huyu huko Fiji anasaidia kusafisha kanisani! Je, wewe unasaidiaje?

Kwa Pamoja

Picha
dad, mom, and son eating together

Familia mara kwa mara hula magimbi, mihogo au matunda ya kitropiki pamoja na mlo wao. Tamu!

Michezo

Picha
boy running with rugby ball

Ragbi ni mchezo maarufu. Ni mchezo wa taifa la Fiji!

Wanyama Marafiki

Picha
picture of an iguana

Fiji ina mimea mingi na wanyama wengi wa kuvutia, kama vile mjusi mabaka.

Hekalu Zuri

Picha
photo of the temple in Fiji

Fiji ina waumini wa Kanisa wapatao 22,000. Ina hekalu huko Suva, ambako ni mji mkuu.

Vielelezo na Katie McDee

Chapisha