2022
Malengo ya Ubatizo
Machi/Aprili 2022


Imeandikwa na Wewe

Malengo ya Ubatizo

Picha
girl watching conference and reading scriptures

Mnamo Novemba 2019, nilimsikiliza Mzee Gong kwenye tukio la Uso kwa Uso kuhusu programu ya Watoto na Vijana pamoja na familia yangu. Baada ya hapo, askofu wangu alitupatia vijitabu vya kutusaidia kufikia malengo yetu.

Lengo langu la kwanza lilikuwa kumaliza kusoma Kitabu cha Mormoni kabla ya kufika miaka minane ili kujiandaa kwa ajili ya ubatizo wangu. Nilikuwa nimekwisha anza kukisoma lakini pasipo hamasa kubwa. Lakini siku hiyo niliandaa mpango na baba yangu. Tulipanga sura za mimi kuzisoma kila siku ili kumaliza Kitabu cha Mormoni kabla ya ubatizo wangu. Nilianza kusoma kila siku na kuweka alama ninapomaliza kusoma kila mlango.

Nilipokuwa ninasoma, nilitaka kufanya mambo mengi mazuri. Hivyo nilijiunga kwenye mfungo wa ulimwenguni kote uliotangazwa na Rais Nelson ili kusaidia kuzuia Uviko-19. Nilifurahia kwamba niliweza kufanya mfungo kamili. Wazazi wangu pia walinihimiza kusali na kufunga ili kupata ushuhuda wangu mwenyewe juu ya Kitabu cha Mormoni na juu ya ubatizo.

Katika Jumapili ya kwanza ya mwezi Mei, nilisali na kufunga. Haikuchukua muda mrefu, nilimaliza kusoma Kitabu cha Mormoni chote. Nilikuwa na furaha kwa ajili ya ubatizo wangu—katika siku yangu ya kuzaliwa. Nilijihisi kuwa niko tayari kufanya agano hili na Mungu! Ninajua kwamba Kitabu cha Mormoni ni cha kweli. Ninapenda kukisoma, na ninayo furaha kwamba nilitimiza lengo hili kwa msaada wa familia yangu.

Vielelezo na Rosalie Ledezma

Chapisha