Kwa Nguvu za Vijana
Je, ni nini Rafiki wa kweli?
Maelezo ya rafiki yamebadilika katika dunia ya leo iliounganishwa kiteknologia. Leo unaweza kufikiri kuwa una “marafiki” wengi. Ni kweli: tunafurahia uwezo wa kuwa na taarifa na kujua kwa usasa yale yanayotokea katika maisha ya wengi wa marafiki zetu na vile vile marafiki wa sasa na wa zamani na hata watu ambao hatujakutana nao kibinafsi tunaowaita marafiki zetu.
Katika muktadha wa vyombo vya habari vya kijamii, neno “rafiki” mara nyingi hutumika kuelezea mawasiliano badala ya mahusiano. Una uwezo wa kutumia “marafiki” zako ujumbe, lakini hii si sawa na kuwa na uhusiano na mtu ana kwa ana.
Wakati mwingine shughuli yetu ni kwa kuwa na marafiki. Pengine tunapaswa kuzingatia kuwa rafiki.
Kuna maelezo mengi ya nini maana ya kuwa rafiki. Kamwe sitawai kusahau kumsikia Mzee Robert D. Hales wa Jamii ya Mitume Kumi na Wawili akizungumza kuhusu maana ya kuwa rafiki na ushawishi wa nguvu ya marafiki katika maisha yetu. Maelezo yake yamekuwa na madhara ya kudumu katika maisha yangu. Alisema, “Marafiki ni watu ambao hufanya kuwa rahisi kuishi Injili ya Yesu Kristo.” Kwa maana hii, kutafuta wema wa juu wa mtu mwingine ni kiini cha urafiki wa kweli. Ni kuweka mtu mwingine kwanza. Ni kuwa madhubuti mwaminifu, mwajibikaji, na mwenye maadili katika kila kitendo. Pengine ni neno ahadi ambalo linafungua maana halisi ya urafiki.
Wakati binti yangu, Emi, alikuwa miaka 15, alifanya uamuzi kuhusu aina gani ya rafiki angeweza kutafuta. Asubuhi moja niliona nakala yake ya Kitabu cha Mormoni imefunguliwa katika Alma 48. Alikuwa ameweka alama mistari iliyomwelezea Kapteni Moroni: “Moroni alikuwa mtu mwenye nguvu na shujaa; alikuwa mtu wa uelewa kamili. Naam, na yeye alikuwa ni mtu ambaye alikuwa imara katika imani ya Kristo” (mistari 11, 13). Katika ukingo alikuwa ameandika, Nataka kufanya miadi na kuolewa na mtu kama Moroni. Nilivyomtazama Emi na aina ya vijana alijihusisha nao na baadaye kufanya miadi alipokuwa miaka 16, ningeona kuwa alikuwa akiiga sifa hizo mwenyewe na kuwasaidia wengine kuishi kwa utambulisho wao kama wana wa Mungu, wamiliki wa ukuhani, na kina baba wa na viongozi wa siku za usoni.
Marafiki wa kweli ushawishi wale ambao wanajihusisha nao kupanda kidogo juu [na] kuwa bora kidogo. Mnaweza kusaidiana, hasa wavulana, kujiandaa kwa ajili ya kuhudumu misheni ya heshima. Mnaweza kusaidiana kubaki wasafi kimaadili. Ushawishi wako mwema na urafiki unaweza kuwa na athari ya milele si tu katika maisha ya wale ambao unajihusisha nao lakini pia kwa ajili ya vizazi vijavyo.
Mwokozi aliwaita wanafunzi Wake marafiki. Yeye alisema.
“Hii ni amri yangu, Mpendane, kama nilivyowapenda ninyi.
“Hakuna mtu aliye na upendo kumshinda huyu, kwamba autoe hai wake kwa sababu ya marafiki zake.
“Ninyi ni marafiki zangu, ikiwa nyinyi mnafanya ninayowaamuru.
“Siwaiti tena watumishi, maana mtumishi hajui anachofanya bwana wake, lakini ninyi nimewaita marafiki; kwa kuwa yote niliyoyasikia kwa Baba yangu mimi nimewajulisha ninyi” (Yohana 15:12–15; mkazo imeongezewa).
Unapoishi na kushiriki injili ya Yesu Kristo, utawavutia watu kwako ambao watataka kuwa marafiki zako—si tu mtu kwenye tovuti ya kijamii lakini ile aina ya rafiki Mwokozi alielekezea kwa maneno yake na mfano wake. Unapojitahidi kuwa rafiki kwa watu wengine na kuwacha nuru yako iangaze sana, ushawishi wako utabariki maisha ya wengi ambao unajihusisha nao. Najua kuwa unapolenga kuwa rafiki kwa watu wengine, kama inavyoelezwa na manabii na mifano katika maandiko, utakuwa na furaha na utakuwa ushawishi kwa ajili ya wema duniani, na siku moja utapokea ahadi tukufu iliotajwa katika maandiko kuhusu urafiki wa kweli: “Uhusiano huu huu uliopo miongoni mwetu hapa utakuwepo miongoni mwetu kule, isipokuwa utazidishwa utukufu wa milele” (M&M 130:2).