Kuwafuata Manabii na Mitume
Mungu huwaita manabii na mitume ili watufundishe kile ambacho Mungu anataka tujue. Katika maandiko tunasoma kuhusu manabii kama Nuhu, Nefi, na Joseph Smith, na mitume kama Petro na Paulo. Tunao manabii na mitume leo!
“Nabii, muonaji, na mfunuzi” ni nini?
Nabii husema kwa niaba ya Mungu.
Muonaji anaweza kujua yaliyopita, ya sasa, na ya siku za usoni.
Mfunuzi anafunua (au anatuonyesha) mapenzi ya Mungu.
-
Washiriki wa Urais wa Kwanza wote ni manabii, waonaji, na wafunuzi. Na hivyo kwa Mitume wote.
-
Ni Rais wa Kanisa pekee aliye na mamlaka kutoka kwa Mungu kuongoza Kanisa zima.
-
Ni manabii, waonaji, na wafunuzi wangapi walio hai tulio nao kwa ujumla?
12 15 3 1
Jibu: 15
Kwa nini ni muhimu kumfuata nabii?
Nabii ni kama mtu ambaye anayelinda kutoka juu ya mnara (ona pia ukurasa wa 38) Anaweza kuona hatari inayokaribia na kutueleza jinsi tunavyoweza kujikinga. Anatusaidia kumfuata Yesu Kristo.
Ni nini nabii wetu ametuagiza tufanye.
Nabii wetu leo ni Rais Thomas S. Monson. Hapa kuna mambo kadhaa ametuomba tufanye.
-
Tufuate mfano wa Yesu Kristo na tumpende kila mtu.
-
Tulipe zaka na tuchangie hazina ya mmisionari.
-
Tuepukane na sinema mbaya, Televisheni na vyombo vingine vya habari.
-
Tuweke picha ya hekalu katika kila chumba cha kulala.
-
Tujifunze hotuba za mkutano mkuu.
-
Tuwatembelee wazee na tuwe majirani wema.
Chagua kitu kimoja kutoka katika orodha hii ambacho unaweza kufanya mwezi huu. Utafanya nini?