Maswali na Majibu
“Ninakejeliwa shuleni kwa kuwa MSM. Ninajua ninapaswa kutetea ninachoamini, lakini ni vigumu sana! Ni namna gani naweza kuwa mjasiri vya kutosha?”
Uko sawa kuwa unahitaji ushujaa ili kukabiliana na hali hii. Hata hivyo, Yesu Kristo ameamuru kuwa, “Inukeni na mng’are, ili nuru yenu ipate kuwa bendera kwa ajili ya mataifa” (M&M 115:5). Lakini kuwa na ujasiri wa kuacha nuru yako ing’are yaweza kuwa na au isiwe na maana kuwa utetee msimamo wako kwa wale wanaokukejeli.
Katika hali yoyote ile, waweza kukubali upinzani kukupa msukumo ili uwe bora. Unapofanya jitihadi kuimarisha ushuhuda wako, unaweza kukuza aina ya ujasiri mtulivu utakaokusaidia kuzungumza au kuendelea tu kufanya kile kilicho haki, hata ikiwa wengine watakukejeli.
Kuchokozwa kunaweza fadhaisha, lakini kumbuka kuwa unaweza kuomba ili ujawe na hisani ili wengine waweze kuhisi upendo wa Kristo kupitia kwako (ona Moroni 7:48). Kwa sababu kila hali ni ya kipekee, tafuta uongozi wa Roho kujua jinsi ya kujibu kama Kristo katika kila hali.
Kutegemea na hali, yaweza kuwa vyema kuzungumza na wale ambao wamekufanyia mzaha kwa faragha au hata kupuuzilia mbali dhihaki huku ukiendelea kuishi kulingana msimamo wako. Ikiwa wengine hawana moyo wa kutaka kusikiliza uliyonayo ya kusema, mfano wako wa ukarimu, kusamehe, na uaminifu wako unaweza kuwa ujumbe bora unaoweza kuwapa.
Onyesha Ujasiri wa Kweli
Wale ambao hukufanyia mzaha wanaweza kosa kusita kufanya hivyo hata ukiwa mjasiri kiasi cha kuwauliza wakome, lakini wanaweza koma unapofanya jitihadi kwa kuishi kile ulicho—Mtakatifu wa Siku za Mwisho. Punde, nuru ya idhini ya Baba yetu wa Mbinguni itang’aa juu yako, kwa matumaini ikifungua macho yao kwa injili ya urejesho maishani mwako.
Bright U., umri 17, Imo State, Nigeria
Pata Nguvu katika Mambo ya Msingi
Maombi na kufunga ni muhimu kwa sababu itakusaidia kukabiliana na mzaha na changamoto shuleni, kama vile Yesu Kristo alikumbwa na dhihaki nyingi alipokuwa hapa duniani. Itakusaidia kuwa na upendo zaidi na subira kwa watu.
Walter C., umri 15, Jaén, Peru
Ongozwa kupitia kwa Maombi
Kwa muda mrefu nilikuwa muumini wa pekee katika shule yangu. Marafiki zangu wa karibu walionekana kunielewa, lakini marafiki wengine shuleni walinifanyia mzaha. Siku moja nilisali na nikahisi kwamba nilihitaji kuzungumza na mmoja wao ambaye alikuwa akiwashawishi wenzake kunifanyia mzaha. Nilimwelezea kwamba sikuwa nimekasirishwa naye, lakini nilimtaka anipe heshima sawa na jinsi ambavyo angetaka kuheshimiwa. Baada ya kusikia mazungumzo yetu, mmoja wa walimu wetu alinitetea kila mara alipoona chochote kikifanyika. Ninajua kwamba Bwana atakuwa nawe unapozungumza na hawa watu.
Shanela S., umri 14, Pangasinan, Philippines
Jenga Ushuhuda Wako
Kwanza, pata ushuhuda wa kweli kuhusu ukweli unaotaka kushiriki na wengine. Kisha uwe na upendo kwa wale watu wanaokufanyia mzaha na usijiingize kwenye mabishano, kwa sababu ukinzani hauungwi mkono na Mungu (ona 3 Nefi 11:29). Cha muhimu kabisa, jitahidi kuwa Roho awe pamoja nawe daima. Roho atakusaidia kuwa na upendo zaidi na ujasiri zaidi, na atafanya maneno yako yawe na nguvu.
Julia F., umri 19, Hesse, Germany
Wapende Maadui Zako
Nimekuwa katika hali sawa kama hizo. Ukiwa na imani na ujinyenyekeze, utabarikiwa na nguvu na imani unayohitaji “kuwapenda maadui zako, kuwabariki wale wanaokulaani, … na kuwaombea” (Mathayo 5:44). Ningekuhimiza upekue maandiko ili upate mjibu kuhusu jinsi unavyoweza kuwa imara. Omba wakati unapohisi upweke katika imani yako. Warumi 8:31 inasema, “Basi, tuseme nini juu ya hayo? Mungu akiwapo upande wetu, ni nani aliye juu yetu?” Uko na Mungu kukutetea! Chochote chawezekana.
Matthew T., umri 15, Utah, Marekani
Msiwe na Hofu
Zungumzeni kuhusu dini yenu kila mara au fanyeni mambo makusudi ili hilo lifanyike. Nilikuwa katika hali sawa na nikaandika, “Ninafurahi kuwa MSM” kwenye mkoba wangu. Kwa kufanya hivyo, nilifungua mlango kwa nafasi kadhaa za umisionari na kuwaonyesha watu kuwa sikuwa na hofu kuwajulisha mimi ni MSM. Chochote utakachofanya, usikubali wakuvunje moyo. Waombee na ujiombee. Punde utagundua kwamba ikiwa lengo lako litakuwa kuokoa nafsi za wengine, hautakuwa na hofu sana kuwaambia ukweli kuhusu injili ya Baba yetu.
Savanna P., umri 14, Texas, Marekani
Ujasiri wa Msimamo Wetu
“Kila mara ni vigumu kuwa tofauti na kusimama pekee yetu kulinda kile tunachoamini katika umati. Ni kawaida kuogopa kile wengine wanaweza kufikiria au kusema. Maneno ya kufariji ya Zaburi: ‘Bwana ni nuru yangu na wokovu wangu, nimwogope nani? Bwana ni ngome ya uzima wangu nimhofu nani?’ [Zaburi 27:1]. Tunapomfanya Kristo lengo la maisha yetu, woga wetu utabadilishwa na ujasiri wa msimamo wetu.”
Rais Thomas S. Monson, “Kuwa Mfano na Nuru,” Liahona, Nov. 2015, 88.
Swali Linalokuja
“Nitajuaje Mungu anasikiliza maombi yangu?”
Wasilisha majibu yako, na ukipenda, picha ya ubora wa hali ya juu kabla ya Mei 1, 2016, katika liahona.lds.org, kupitia barua pepe kwa liahona@ldschurch.org, au kupitia barua pepe (ona anwani katika ukurasa wa 3).
Taarifa ifuatayo na ruhusa lazima ijumuishwe katika barua pepe yako au barua: (1) jina kamili, (2) tarehe ya kuzaliwa, (3) kata au tawi, (4) kigingi au wilaya, (5) ruhusa yako uliyoandika, na kama u chini ya miaka 18, ruhusa iliyoandikwa na mzazi wako (barua pepe inakubalika) ili kuchapisha majibu yako na picha.
Majibu yanaweza kuhaririwa kwa ajili ya urefu au ufafanuzi.