2016
Nenda Ukamsaidie
Aprili 2016


Sauti za Watakatifu wa Siku za Mwisho

Nenda Ukamsaidie

Thomas Robbins, California, Marekani.

woman with kids at the register

Nilisimama kwenye foleni katika kituo cha mafuta. Mbele yangu, mama mwenye watoto wawili wadogo aliagiza petroli ya dola $3 na aiskrimu koni mbili za vanila.

Kwa mtazamo wa niliweza kuona kwamba walikuwa na pesa kidogo sana. Watoto walikuwa miguu mitupu na walikuwa wamevaa nguo zilizochakaa.

Nilimsikia mwanamke yule akiweka kilichoonekana kuwa kiasi kikubwa sana cha sarafu kwenye kaunta kulipa bili yake.

Baada ya kulipia petroli yangu, nilitoka nje na kutupia jicho gari la mama yule. Lilikuwa modeli ya zamani ambayo huenda ilisafiri maili chache sana ikilinganishwa na matumizi ya petroli.

Nilihisi kichomi cha huruma kwa mama huyu wa watoto wawili, lakini niliwasha pikipiki yangu na kuendelea na siku yangu.

Chini ya dakika moja katika safari yangu kwenye barabara kuu, sauti ilinijia: “Nenda ukamsaidie.” Msukumo ulikuja mara mbili.

Nilitingisha kichwa, nikifikiria kuwa huenda alikuwa ameshaondoka tayari. Ni nini ningemwambia hata hivyo?

Sauti ilikuja wazi mara ya tatu: “Nenda ukamsaidie!”

Niligeuka kuelekea kwenye kituo kile cha mafuta, nikijaribu kufikiria kile ningemwambia ikiwa angekuwa bado yuko mahali pale.

Nilipowasili, niliona kwamba milango ya gari lake ilikuwa wazi. Alikuwa kwenye kiti cha dereva, na watoto wake wadogo wawili walikuwa wakifurahia aiskrimu kwenye kiti cha nyuma.

Nilitoa ombi dogo, nikimwomba Baba wa Mbinguni anijulishe kile ambacho ningesema. Sauti iliniambia, “Jitambulishe na uulize ikiwa anahitaji usaidizi.” Nilikaribia gari lake na kujitambulisha. Nilimueleza kuwa nilihisi msukumo wa kumuuliza ikiwa alihitaji usaidizi wowote.

Alianza kulia na kusema, “Nimemaliza tu kumuomba Yesu, nikimwomba atume mtu wa kunisaidia.”

Baba wa Mbinguni alikuwa amejibu maombi yake. Nililipa kujaza mafuta gari lake na nikampa nambari ya simu ya mtu katika akidi yetu ya wazee ambaye alikuwa akiajiri kwa wakati huo. Sijui yaliyomkuta mama yule kijana baadaye, lakini ninashukuru nilifuata msukumo wa kumsaidia.