Yeye ndiye Askofu?
Mtunzi anaishi Illinois, Marekani.
Kwa sababu nilikuwa si mhudhuriaji mzuri miaka iliyopita, muumini aliyenijua mimi wakati huo hakuweza kuamini niliitwa kuwa askofu.
Wakati wa mkutano wa baraza la utendaji la ukuhani, wamisionari wetu waliarifu kukutana na muumini ambaye kumbukumbu zake hazikuwepo katika kata. Nililitambua jina mara lilipotajwa kwamba mimi na yeye tuliwahi kuwa katika kata moja kwa miaka mingi iliyopita.
Mmoja wa wamisionari hao alisema, “Ndiyo, askofu, alisema hilo na alionekana kushangazwa kwamba wewe ni askofu.”
Niliwauliza, “Alisema nini?”
Walisema alionekana kushangazwa sana na alisema, “Yeye ndiye askofu?”
Nilicheka na kueleza kwamba dada huyu alinijua kama mtu tofauti kabisa miaka 30 iliyopita.
Nilipolitafakari jambo hili baadae, niliwaza ni kiasi gani maisha yangu yamebadilika katika kipindi cha miaka 30 na zaidi ambayo mimi na familia yangu tumekuwa waumini. Nimewafahamu waumini wengi wa kata yangu kwa miaka 20 na nimetumikia kama rais wa tawi na kama askofu, lakini hakuna yeyote katika waumini hawa aliyenijua mimi miaka 30 iliyopita. Ingawa mara chache nimesimulia matukio ya maisha yangu ya zamani ili kufundisha toba na Upatanisho wa Yesu Kristo, sehemu kubwa ya kata hawajui safari ngumu ya kushangaza ya maisha yangu katika Kanisa ilivyokuwa.
Familia yangu na mimi tulitambulishwa kwa Kanisa Mei 1979, na nilijua mara moja kwamba hapa ndipo sisi tunapaswa kuwa. Tulibatizwa Juni, na mwanzoni kabisa sote tulikuwa wahudhuriaji wazuri, lakini haikuchukua muda kabla ya mimi kuacha kuhudhuria na kurudi katika tabia zangu za zamani. Kamwe sikuwahi kwa kweli kuwa na shaka kuhusu ukweli juu ya injili na Urejesho, lakini sikuwahi kuwaza kwamba nilikuwa na cha kunifanya kuwa muumini mzuri wa Kanisa.
Mwaka 1982, kwa sababu ya kuendekeza utawaliwa wa ulevi, mke wangu, ambaye kamwe hakuwahi kushindwa katika imani yake, aliomba talaka. Wakati huo familia yangu ilikuwa ikiishi Oklahoma, Marekani, lakini mimi nilirejea Illinois, Marekani, mahali nilikolelewa. Nilifika mahali ambapo nilikuwa karibu kupoteza kitu cha pekee ambacho kwa kweli ni cha thamani kwangu: familia yangu.
Nilianza kusali nikipiga magoti asubuhi na jioni kwa Mungu ambaye sikuwa tena na uhakika kama yupo au kama alikuwepo, nilidhani Yeye amekwisha nisahau muda mrefu uliopita. Lakini kwa miezi mitatu nilisali kwa uaminifu kabisa. Mapema asubuhi moja, wakati nikiwa nimezama katika sala, hisia za usaidizi zikaja juu yangu na nikajua kwamba Mungu anaishi, na kwamba ananijua, na kwamba ananipenda. Pia nilijua sitagusa tena tone jingine la kileo.
Jioni ile ile nilipokea simu kutoka kwa mke wangu akinifahamisha kwamba anatuma makaratasi ya talaka ili niweke saini. Wakati wa mazungumzo hayo ghafla akasema, “Kuna kitu tofauti sana juu yako. Siamini kama utakuja kunywa tena, na nitachana makaratasi haya.” Tukarudiana, na miaka miwili baadae akamzaa mtoto wetu wa tatu wa kiume.
Mtu angefikiri kwamba ningelirudi na kuwa mhudhuriaji mkamilifu katika Kanisa, lakini mimi mwenye kichwa kigumu. Nilirudi kwa muda hata nikapokea wito kuwa mwalimu katika akidi ya wazee. Lakini mara nikaanza kujisikia nisiyetosha kufundisha na tena nikasimama kuwa mhudhuriaji
Katika mwaka 1991 tulihamini katika tawi dogo. Miezi kadhaa kabla ya siku ya kuzaliwa ya mwaka wa nane ya mwana wetu mdogo wa kiume, mke wangu, rais wa Msingi, walimwuliza yeye ni nani angependa afanye ubatizo wake. Ni wazi alitaka baba yake afanye ibada hiyo. Mke wangu akamwambia kwamba yawezekana hiyo haitatokea. Yeye hakukubali jibu hilo na akajitwika jukumu la kumrejesha baba yake. Alikuwa wa kujishughulisha sana, na kwa ufupi nilijikuta nikitumika kama Skautmasta, na baadae nikambatiza na kumthibitisha mwanangu wa kiume.
Miezi minane iliyofuatia baada ya kurudi katika uhudhuriaji kamili kulikuwa na matukio mengi. Tulifunganishwa pamoja kama familia katika Hekalu la Illinois Chicago, na mimi tena nikaitwa kuhudumu kama mwalimu wa akidi ya wazee, lakini wakati sikuacha tena. Kisha niliitwa kuwa mshauri katika urais wa tawi, na miezi mitano baadae nikaitwa kutumikia kama rais wa tawi. Ni mwezi hivi kama sikosei baada ya wito wangu, ninakumbuka kufikiria, “Mimi rais wa tawi?”
Nimewaeleza Watakatifu wengi wanaohangaika kwa miaka mingi kwamba kama mimi nimeendelea katika injili, basi mtu ye yote anaweza. Ni suala tu la kuelewa nguvu halisi za Mwokozi na Upatanisho Wake na kuchukua hatua za kuja Kwake.
Milele nitamshukuru mke wangu na watoto na walimu wote wa nyumbani walio waaminifu, viongozi wa akidi, maaskofu, na Watakatifu walio waaminifu ambao waliweka mfano mwema kwa ajili yangu. Imekuwa fursa nzuri kwangu kumtumikia Bwana na Watakatifu kwa miaka hii 20 iliyopita. Maisha yangu yamebarikiwa kupita cho chote ambacho naweza kufikiria.