2023
Vijana Ethiopia Wanachafua Mikono Yao na Kupanda Miti 200 ya Matunda
Machi 2023


Habari za Eneo

Vijana Ethiopia Wanachafua Mikono Yao na Kupanda Miti 200 ya Matunda

Vijana Ethiopia Wanachafua Mikono Yao na Kupanda Miti 200 ya Matunda.

Yesu Kristo alikua katika nyanja zote za maisha Yake. Kiroho alipata kibali mbele za Mungu, kijamii aliwapendeza wanadamu, kimwili aliongezeka katika kimo na kiakili aliongezeka katika hekima. (Ona Luka 2:52.)

Wakijitahidi kufuata mfano wa Mwokozi Yesu Kristo katika nyanja zote za maisha yao, kwa upekee kijamii na kimwili, takriban vijana 70 wa Ethiopia, Addis Ababa waliungana katika kupanda miti 200 ya matunda.

Juhudi hii ilikuja baada ya Rais wa Misheni ya Ethiopia, Addis Ababa Robert J. Dudfield na Rais wa Tawi la Meganagna, Rais Birhanu Molla kuifikia serikali ya eneo husika kwa ajili ya kuomba fursa ya kuhudumu.

“Tulifika kuona kama kulikuwa na fursa katika eneo na walirejea na tamanio [kwa ajili yetu] kupanda miti ya matunda,” alisema Rais Dudfield.

Rais Dudfield na Rais Molla walisonga mbele kwa kuandaa mkutano wa vijana ambapo vijana wa kanisa, wamisionari na viongozi wa kanisa wa eneo husika kutoka matawi mbalimbali ya Addis Ababa, wakipewa motisha na hamu ya kuacha matokeo ya kudumu katika jumuia, walichukua vifaa vyao vya bustani na kuvipa kazi vidole vyao vya kijani.

Takriban wiki sita za kupanga na kupanda chini ya jua kali la Ethiopia zilileta matokeo ya miti 200 iliyopandwa ya matufaha, ndimu, maembe na avokado.

“[Kwa] matunda kuwa adimu sana na ghali sana Addis Ababa, serikali ya eneo husika ilipongeza juhudi zetu kwa furaha na shukrani. Miti ya matunda itawashibisha wasio na makazi katika jumuia,” Rais Dudfield alisema.

Akishuhudia juu ya matunda ya huduma, Mzee Dylan Gilman, Mmisionari anayehudumu Addis Ababa alisema kwamba fursa ya kuhudumu imesaidia kuwaunganisha vijana.

“Ilikuwa ya kupendeza kuwaona vijana wakija pamoja ili kuisaidia jumuia. Kupanda miti ya matunda [ulikuwa] uzoefu wa kuinua, hasa kuwaona vijana wakipata fursa ya kuwa wamoja wakati wakiwahudumia wengine. Ethiopia hakika imebarikiwa kwa kundi la vijana la kupendeza,” Mzee Gilman alisema.

Hana Debebe Hailu, kijana kutoka Tawi la Megenagna, alielezea shukrani zake juu ya matokeo ya kuhudumu wakati wa mradi.

“Nilipenda jinsi tulivyokuwa kwenye kundi moja wakati wa shughuli, ilikuwa ya kupendeza pia kumwona kila mmoja wetu tukisaidiana. Nilikutana na watu wengi na niliwaona rafiki zangu. Nilifurahi sana kuhusu uzoefu na somo la kujifunza pia. Somo lilinifanya nihisi vizuri kwa sababu lilikuwa kuhusu Mungu, kuhudumiana na kupendana. Kamwe sitasahau uzoefu huu.”

Kijana mwingine, Moti Tegegn Lemma kutoka Tawi la Summit, alifunguka kuhusu jinsi huduma ya miti ya matunda ilivyomsaidia kukua kijamii.

“Katika shughuli ya huduma nimejifunza mambo mengi, siwezi kuhesabu ni mangapi. Nimeweza kukutana na marafiki wengi na nina shukrani nyingi kwa Mungu kwa kunisaidia kuweza kupata muda wa kufanya huduma na kuwasaidia wengine,” Moti alifunguka.

Mji mkuu wa Ethiopia Addis Ababa una jumla ya idadi ya waumini wanaokua 1,943, matawi 5, kituo kimoja cha historia ya familia na misheni moja. Rais Robert na Dada Darice Dudfield ni viongozi wa kwanza wa misheni kusimamia misheni ya Ethiopia Addis Ababa. Misheni ilitangazwa kwa mara ya kwanza mnamo Novemba 2019 na kufunguliwa mnamo Julai 2020.