“Tumeungana kama akina Dada na akina Kaka katika Kristo,” Liahona, Sept. 2023.
Karibu kwenye Toleo Hili
Tumeungana kama akina Dada na akina Kaka katika Kristo
Sauti za wote wanawake na wanaume ni muhimu ili kutimiza kazi ya Bwana. Ingawa ni kipekee, tunakamilishana, tunaunganika katika lengo letu la pamoja la kuwa wafuasi wa Kristo.
Tofauti zetu hazifai kututoa kwenye lengo hili. Badala yake, tofauti zetu hujumuisha talanta zetu na michango ambayo kwa pamoja huimarisha matokeo yetu katika kazi ya duniani kote ya wokovu na kuinuliwa. Mzee Gerrit W. Gong wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili anaandika katika toleo hili, “Tunafikia maamuzi bora na kuwa na ufanisi mkuu katika huduma ya Bwana tunapothamini michango ya kila mmoja na kufanya kazi pamoja, akina kaka na akina dada katika kazi Yake” (ukurasa wa 4). Ni kwa jinsi gani tunapata umoja kama huu? Ni sharti tuwe na imani kwamba Bwana anaweza kufanya kazi kwa tofauti zetu kwa ajili ya wema katika ufalme Wake.
Katika makala yangu kwenye ukurasa wa 8, ninashiriki kile ambacho nimejifunza kutoka kwenye tukio la Agano Jipya la mwanamke wa Kanaani, ambaye alimtafuta Mwokozi amponye binti yake. Mwanamke huyu hakuwa wa nyumba ya Israeli. Lakini yeye alikuwa na imani kwamba nguvu za Mwokozi zingemponya mtoto wake, na hii imani ya ajabu ilimuunganisha na watu wa agano na kuleta muujiza.
Na tumtegemee Mwokozi katika yote tunayofanya, kwa “mioyo yetu ikiwa imeungana pamoja katika umoja na katika kupendana” (Mosia 18:21). Tumepata upendeleo wa kujifunza kutoka kwenye tofauti zenye nguvu za mmoja na mwingine na kuzithamini kama Kristo anavyofanya. Nina shukrani jinsi gani kuwa na mchungaji ambaye husikia sauti za kipekee za kila mmoja wa kondoo Wake.
Kwa moyo wa dhati,
Dada Camille N. Johnson
Rais Mkuu wa Muungano wa Usaidizi