“Taipei, Taiwan,” Liahona, Sept. 2023.
Kanisa Liko Hapa
Taipei, Taiwan
Jumba la mikutano ya ibada la kwanza la Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho huko Taiwan, lilikamilika mnamo 1966, lilijengwa katika mji mkuu wa Taipei na waumini wenyeji. Leo, Kanisa huko Taiwan lina:
-
Waumini 62,100 (kwa makadirio)
-
Vigingi 16, kata na matawi 98, misheni 2
-
Hekalu 1 katika Taipei, I lilitangazwa huko Kaohsiung
Kwenda Hekaluni
Familia ya Ruan inatembea kwenye bustani za hekalu katika Taipei. Dada Ruan anasema, “Kwenda hekaluni hunikumbusha vipaumbele katika maisha na hunipa nguvu za kiroho na kuhisi amani.” Katika mkutano mkuu wa Oktoba 2021, Rais Russell M. Nelson alitangaza kwamba hekalu la pili lingejengwa katika Kaohsiung.
Zaidi kuhusu Kanisa huko Taiwan
-
Historia fupi ya Kanisa huko Taiwan.
-
Mmisionari huko Taiwan anajifunza kuhusu thamani yake mwenyewe kutoka kwenye sanamu maarufu, Jadeite Cabbage.
-
Mtaiwani mtangulizi anajifunza kuheshimu nasaba yake huku akishika amri.
-
Uhudumiaji kwa upendo safi, waumini wa kata wanamsaidia Ken kurudi kanisani.
-
Licha ya mashinikizo ya kijamii, Han Lin anafanya kazi kwa bidii tangu ujana wake ili kuwa baba mwema.
-
Iren na Yéyé Iren na Yéyé wanajifunza kuwaheshimu watu wengine na dini zingine walipokuwa wanatembelea hekalu la Buddha pamoja na babu yao.
-
Kusoma maandiko kuhusu Mwokozi huleta amani kwa vijana hawa.