“Nyaraka za Mtume Paulo, Sehemu ya 2,” Liahona, Sept. 2023.
Njoo, Unifuate
Nyaraka za Mtume Paulo
Sehemu ya 2
Waefeso
-
Kwa waumini wa Kanisa katika Efeso (mji katika Uturuki ya sasa)
-
Uliandikwa kutoka Rumi karibia 60–62 BK
-
Dhumuni: Kuwafundisha waongofu, kuhamasisha umoja, na kuwatia moyo Watakatifu kuvumilia dhidi ya uovu.
-
Mafundisho muhimu: Kipindi cha ujalivu wa nyakati, wokovu kwa neema, kuanzisha na dhumuni la Kanisa, na utaratibu katika maisha ya familia
Wafilipi
-
Kwa waumini wa Filipi (mji katika Ugiriki ya sasa)
-
Uliandikwa kutoka Rumi karibia 60–62 BK
-
Dhumuni: Kuwasifia Watakatifu kwa ajili ya imani yao na dhabihu na kuwaonya Wakristo mafisadi.
-
Mafundisho muhimu: Kanuni za kuishi kwa haki, kumtegemea Kristo kwa ajili ya wokovu, na kufanya dhabihu kwa ajili ya injili
Wakolosai
-
Kwa waumini katika Kolosai (mji katika Uturuki ya sasa)
-
Uliandikwa kutoka Rumi karibia 60–62 BK
-
Dhumuni: Kuwaonya wenye kiburi na kutilia mkazo kwamba ukombozi huja kupitia Kristo
-
Mafundisho muhimu: Asili ya Kristo, kujenga msingi juu Yake na kukuza sifa kama za Kristo.
1 Wathesalonike
-
Kwa waumini katika Thesalonike (mji katika Ugiriki ya sasa)
-
Uliandikwa kutoka Korintho (mji katika Ugiriki ya sasa)
-
Dhumuni: Kutoa himizo na kujibu maswali kuhusu Ujio wa Pili
-
Mafundisho muhimu: Kupendana, Ufufuko, na Ujio wa Pili
2 Wathesalonike
-
Kwa waumini katika Thesalonike (mji katika Ugiriki ya sasa)
-
Uliandikwa kutoka Korintho (mji katika Ugiriki ya sasa)
-
Dhumuni: Kuimarisha imani na kufafanua kutoeleweka kwa Ujio wa Pili
-
Mafundisho muhimu: Hatima ya waovu, Ukengeufu Mkuu na umuhimu wa kufanya kazi kukidhi mahitaji ya kimwili