“Safari za Mtume Paulo,” Liahona, Sept. 2023.
Njoo, Unifuate
Safari za Mtume Paulo
Paulo alianza safari nne muhimu za umisonari, akisafiri karibu maili 9,150 (km 14,725) katika miaka 14. Utayari wake wa kusafiri umbali mkubwa ili kuhubiri juu ya Kristo ulisaidia kuanzisha Ukristo kote katika Mediterania.
Safari Nne za Umisionari za Paulo
Safari ya Kwanza (ona Matendo ya Mitume 13:1–14:28)
-
Muda: takriban 47–49 BK
-
Aliandamana na: Barnaba na Yohana Marko
-
Mwisho wa Safari: Kipro, Uturuki
-
Umbali: karibia maili 1,400 (km 2,250)
Safari ya Pili (ona Matendo ya Mitume 15:36–18:22)
-
Muda: takriban 50–53 BK
-
Aliandamana na: Sila, Timotheo, Prisila na Akila, na Luka
-
Mwisho wa Safari: Shamu, Uturuki, Ugiriki, Yerusalemu
-
Umbali: karibia maili 2,800 (km 4,500)
Safari ya Tatu (ona Matendo ya Mitume 18:23–21:15)
-
Muda: takriban 54–58 BK
-
Aliambatana na: Timotheo, Luka, na wengine
-
Mwisho wa Safari: Uturuki, Ugiriki, Lebanoni, Israeli
-
Umbali: karibia maili 2,700 (km 4,350)
Safari ya Nne (ona Matendo ya Mitume 27:1–28:16)
-
Muda: takriban 59–60 BK
-
Aliandamana na: walinzi Warumi, Luka, na wengine
-
Mwisho wa Safari: Israeli, Lebanoni, Uturuki, Krete, Malta, Sisili, Rumi
-
Umbali: karibia maili 2,250 (km 3,600)