2021
Kulingasha Historia ya Familia
Novemba/Desemba 2021


Kitu cha kufurahisha

Kulinganisha Historia ya Familia

Picha
girl playing matching games with pictures of her family

Eva anatoka Urusi. Anapenda kufanya shughuli za historia ya familia! Anatengeneza picha za video ili kushirikisha mawazo yake pamoja na wengine. Hapa ni mojawapo unayoweza kujaribu.

  1. Chora au chapisha picha mbili za kila mwanafamilia—moja wakati wakiwa wadogo na moja wakati wakiwa wakubwa.

  2. Zigundishe picha hizo kwenye karatasi nzito. Paka rangi nyuma ya karatasi hiyo. (Eva alipamba yake kwa rangi ya maji)! Kisha ziondoe picha kwa kuzikata ili kutengeneza kadi.

  3. Sasa cheza mchezo wa kuzifananisha! Ziweke kadi hizo uso ukiangalia chini. Chukua kadi mbili. Kama zinaonesha watu tofauti, zirudishe. Kama zinaonesha mtu yule yule, zitunze kadi na rudia tena. Ni milingano mingapi unayoweza kuipata?

Picha
Friend, November 2021 Tier 2

Chapisha