2021
Yesu Aliwaheshimu Wazazi Wake
Novemba/Desemba 2021


Kusaidia Kama Yesu

Yesu Aliwaheshimu Wazazi Wake

Picha
young Jesus with his parents

Kuwaheshimu wazazi wako inamaanisha kuwapenda, kuwaheshimu, na kuwatii. Yesu aliwaheshimu wazazi Wake, Mariamu na Yusufu, hapa duniani. Pia alimheshimu Baba Yake wa mbinguni kwa kushika amri.

Alipozidi kukua, Yesu aliwatii wazazi Wake wa kidunia. Aliwapenda na kuwatunza. Hata wakati Alipokuwa anakufa msalabani, Alimwomba mmoja wa wanafunzi wake kumtunza mama Yake.

Picha
boy reading to his brother

Ninasaidia kuweka chumba changu katika hali ya usafi. Pia namsaidia mama kuandaa meza kwa ajili ya kifungua kinywa, chakula cha mchana, na jioni. Ninasaidia na wanyama wa kufuga, kuokota wanasesere wangu, na kumwangalia kaka yangu mdogo.

Sebastiani V., umri miaka 7, Kitengo cha Kati, Paraguay

Picha
Friend, November 2021 Tier 2

Kielelezo na Andrew Bosley

Chapisha