Onyesha na Elezea
Wakati ninapofikiri kuhusu hekalu, ninakuwa na hisia nzuri. Nangojea kwa hamu kuwa na umri wa miaka 11 na kuhudumia katika hekalu la Baba wa Mbinguni.
Rafael D., umri miaka 10, Paraná, Brazil
Mti wangu wa familia unaonekana mzuri kwa sababu una majina na picha za mababu na mabibi zangu na ndugu juu yake. Nimefanya faharasa za majina 1,156! Ninaamini kufanya faharasa ni njia ya kuleta familia pamoja.
Grace D., umri miaka 11, Mkoa wa Greater Accra, Ghana
Kijana mgeni alihamia kwenye darasa la shule yetu katikati ya mwaka. Nilijitolea kumsaidia ajione amekaribishwa. Yeye ni mmoja wa marafiki zangu wapya!
Connor E., umri miaka 7, Mazovia, Poland
Nilizaliwa Guatemala, na kwa Día de Muertos. Siku ya Wafu, watu hutengeneza tiara ili kuwakumbusha juu ya wanafamilia wao waliofariki. Nilitengeneza tiara yenye picha za mababu zangu na picha yangu mwenyewe katikati ili kunikumbusha mapenzi yao.
Sienna S., umri miaka 8, Utah, Marekani
Nilisaidia kupeleka kuni kwa familia ili waweze kupata joto ndani ya nyumba yao.
Sebastian B., umri miaka 10, Virginia, Marekani
Tulisaidia kwenye stoo ya chakula kwa kupakia maboksi ya chakula. Ilitukumbusha kuwa na shukrani kwa kile tulichonacho. Tulihisi furaha kwani tuliweza kuhudumia pamoja na kata yetu.
Emma K. na Charlotte F., umri miaka 9 na 11, New Jersey, Marekani
Wakati Rais Nelson alipotuomba kusoma Kitabu cha Mormoni, niliamua kukisoma pamoja na wazazi wangu. Nilimhisi Roho Mtakatifu akiniambia Kitabu cha Mormoni ni cha kweli. Nimekuwa nikisoma maandiko yangu kila siku na nimepata ushuhuda wenye nguvu zaidi.
Savanna P., umri miaka 10, Texas, Marekani
“Kristo Anatupenda,” Andrea V., umri miaka 8, Retalhuleu, Guatemala
Emma C., umri miaka 7, Santiago, Chile
“Toa Shukrani,” Lincoln H., umri miaka 10, Idaho,Marekani
“Yona na Nyangumi,” Ben M., umri miaka 10, Missouri, Marekani
Babby H., umri miaka 8, Alberta, Canada