2021
Tayari kwa ajili ya Hekalu
Novemba/Desemba 2021


Tayari kwa ajili ya Hekalu

Hadithi hii ilitokea huko Jamaica.

“Nawezaje kupata kibali? Ajan aliuliza.

“Hakikisheni kwamba mnafanya vitu vyote kwa ustahilifu” (Mormoni 9:29).

Picha
family meeting together at home in Jamaica

Ajan alitoa tabasamu kubwa aliposikia hodi mlangoni. Madda (Mama) amemwalika kaka yao mtumishi ili kusaidia mkutano maalumu wa nyumbani jioni.

Yeye alifungua mlango. “Wah gwaan, Kaka Williams!” (“Mambo vipi?”)

Kila kitu safi!” Kaka Williams alisema. (“Kila kitu kiko sawa!”) Alimpa Ajan mfuko wa maembe kutoka kwenye mti wake.

Kaka Williams aliketi kwenye kochi. Madda alimwomba dada mdogo wa Ajan, Dana, kusali.

Baada ya kumaliza, Kaka Williams alisema, “Mwaka huu Ajan atakuwa na umri wa miaka 12. Kuna yeyote anayejua kwa nini mwaka huu ni muhimu kwake”?

Mdogo wa Ajan, Tejaun, alisisimka kwa shauku. “Kwa sababu anaweza kupata ukuhani na kupitisha sakrament!”

“Hiyo ni sawa!” Kaka Williams alisema. “Lakini kuna sababu nyingine pia.

Alifungua pochi yake na kutoa kipande kidogo cha karatasi. “Hiki ni kibali cha hekaluni.”

Alimpa Ajan.

“Asante!” Ajan alipapasa kwa vidole vyake hekalu la dhahabu kwenye kadi. “Unafanya nini na kibali hiki?”

“Ninakionesha kwa mtu aliyekaa mapokezi hekaluni. Inawaonyesha wao kwamba ninastahili kuingia ndani.”

“Nataka kukiona!” Danna alikinyakuwa kutoka kwa Ajan na kukisoma kwa ukaribu.

“Unafikiri utajisikiaje kama ungekuwa na kibali chako mwenyewe?” Kaka Williams aliuliza.

“Nitajisikia mtu muhimu!” Ajan aliangalia juu kutoka kwenye kadi. “Lakini sijui kama ninaweza kwenda hekaluni. Ni gharama kubwa kununua tiketi ya ndege kwenda kule.”

“Hata mimi siwezi kwenda hekaluni mara kwa mara ,” Kaka Williams alisema. “Lakini kibali changu kinanikumbusha siku zote niwe tayari kuingia ndani.”

Ajan alifikiri kwa dakika chache. “Ninataka kuwa tayari pia,” alisema “Nawezaje kupata kibali?”

“Unakutana na askofu,” Kaka Williams alisema. “Atakuuliza maswali kadhaa ili kuona kama wewe upo tayari.”

“Kwa hiyo ni kama kupimwa?” Ajan aliuliza kwa wasiwasi.

“Kwa zaidi ni kama mazungumzo,” Kaka Williams alisema. “ Askofu ni rafiki yako, na anataka kukusaidia uwe tayari.”

Ajan alikubali kwa kichwa. Alimpenda askofu.

“Ungependa kuyaona maswali hayo?” Kaka Williams alimpa Ajan kipande cha karatasi chenye maswali juu yake. Dana na Tejaun walibanana kumzunguka waone pia.

“Namba moja,” Ajan alisoma “‘Je, una imani katika na ushuhuda juu ya Mungu, Baba wa Milele; Mwanaye, Yesu Kristo; na Roho Mtakatifu?’”

Alichangamka. Hilo lilikuwa rahisi. “Ndiyo!”

Aliendelea kusoma maswali, moja baada ya jingine. Madda na Kaka Williams walielezea baadhi ya vitu vilimaanisha nini.

Kisha Ajan alisoma swali jingine: “Unaelewa na kutii Neno la Hekima?” Alikunja uso. “Wakati mmoja D’andre alinipa panchi iliyotengenezwa na kinywaji kikali nilipokuwa nyumbani kwake.” alisema “Lakini kamwe sitaki kuinywa tena. Je, hiyo inamaanisha siwezi kuwa na kibali cha hekaluni?”

“Kutii Neno la Hekima inamaana kutokunywa kilevi, na panchi ina kilevi ndani yake,” Kaka Williams alisema. “Lakini unaweza siku zote kutubu na kwa kustahili kwenda hekaluni.”

“Kwa sababu ya Yesu!” alisema Tejaun.

“Kabisa!” Kaka Williams alisema. “Kisha kibali chako cha hekaluni kinaweza kukukumbusha kuendelea kutii Neno la Hekima. Na daima kuwa tayari kwenda hekaluni.”

Ajan alitabasamu. Alijisikia vizuri sana.

“Pengine nitapata kwenda hekaluni wakati fulani hivi karibuni,” Ajan alisema. “Na nitakapofanya hilo, nitakuwa tayari!”

Picha
Friend, November 2021 Tier 2

Kielelezo na Shawna J. C. Tenney

Chapisha