2021
Kutana na Magali kutoka Uruguay
Novemba/Desemba 2021


Mikono Saidizi Ulimwenguni Kote

Kutana na Magali kutoka Uruguay

Kutana na watoto wa Msingi wakiwasaidia wengine, kama Yesu alivyofanya.

Picha
picture of Magali

Yote kuhusu Magali

Picha
pictures of Magali’s favorite things

Miaka: 11

Kutoka: Uruguay

Lugha: Kihispania

Familia: Baba, Mama, kaka mmoja, dada wawili, na Bibi

Malengo na Ndoto: 1) Kwenda misheni. 2) Kufanya kazi na UNICEF ili kuwasaidia watoto ulimwengu mzima.

Mikono Saidizi ya Magali

Picha
Magali helping feed cows on farm

Magali anawasaidia wazazi wake kwenye shamba lao. Anakusanya mayai ya kuku kwa ajili ya famila yake kuyala. Anawapa ndama maziwa na kuwanywesha maji sungura. Kusaidia familia yake kumemfundisha kwamba huduma ni kitu muhimu sana. Magali anasema, “Siku zote tunapaswa kuwatumikia wale wanaotuzunguka.”

Njia nyingine Magali anayotumikia ni kwa kumsaidia bibi kusoma maandiko, hususani Kitabu cha Mormoni. Ana furaha sana kwa kumfuata Yesu kwa kuwasaidia wengine.

Mambo Ayapendayo Magali

Mahali: Hekalu la Montevideo Uruguay

Hadithi kuhusu Yesu: Wakati Yesu alipomponya mwanamke aliyegusa vazi lake

Wimbo wa Msingi: “When I Am Baptized” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 103)

Chakula: Kila kitu mama yake anachopika

Rangi: Pinki

Somo shuleni: Hisabati

Picha
Friend, November 2021 Tier 2

Vielelezo na Tammie Lyon

Chapisha