2021
Wananisubiri Mimi!
Novemba/Desemba 2021

Imeandikwa na Wewe

Wananisubiri Mimi!

Siwezi kungojea kubatizwa kwa ajili ya mababu zangu!

Picha
photo of two girls and mom in India

Mambo! Jina langu ni Giselle Olivia. Nilizaliwa India. Mimi nampenda Kristo. Asilimia 2.3 ya watu wa India ni Wakristo. Ndio, ni vigumu wakati mwingine. Lakini ninajua Ananisaidia na kuniongoza. Na sasa Kanisa linajenga hekalu India!

Ninaishi katika jiji zuri pamoja na mamilioni ya watu. Miongoni mwa mamilioni yote, kuna watu sita ninaowapenda mno: mama yangu; dada yangu mdogo, Halle; wapendwa bibi na babu yangu; mjomba wangu; na shangazi yangu. Wao ni watu muhimu mno katika maisha yangu.

Mwaka huu tulifanya baadhi ya shughuli za historia ya familia, na nikajifunza kuhusu mababu zangu. Mama alisema wote wanawake na wanaume katika familia walikuwa na nywele ndefu sana, kama vile mimi. Kisha alisema kitu kimoja muhimu sana: mababu zangu wananisubiri katika ulimwengu wa kiroho! Alisema kwamba wanasubiri kubatizwa—kama vile ilivyonibidi kusubiri mpaka nilipokuwa na umri wa miaka minane ili kubatizwa. (Licha ya hayo, nilibatizwa katika kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa kwangu! Safi, siyo?)

Mama alisema mababu zangu wako katika ulimwengu wa kiroho. Hawana miili kama mimi, kwa hiyo hawawezi kubatizwa. Inasikitisha sana! Ndio sababu sisi tunatakiwa kubatizwa kwa ajili yao hekaluni. Nilimwambia Mama kwamba mara hekalu litakapokuwa limejengwa Bengaluru, na mara nitakapokuwa na umri mkubwa wa kutosha, ninataka kubatizwa kwa ajili yao.

Picha
drawing of future temple in India

Mambo! Jina langu ni Giselle Olivia. Nilizaliwa India. Mimi nampenda Kristo. Asilimia 2.3 ya watu wa India ni Wakristo. Ndio, ni vigumu wakati mwingine. Lakini ninajua Ananisaidia na kuniongoza. Na sasa Kanisa linajenga hekalu India!

Ninaishi katika jiji zuri pamoja na mamilioni ya watu. Miongoni mwa mamilioni yote, kuna watu sita ninaowapenda mno: mama yangu; dada yangu mdogo, Halle; wapendwa bibi na babu yangu; mjomba wangu; na shangazi yangu. Wao ni watu muhimu mno katika maisha yangu.

Mwaka huu tulifanya baadhi ya shughuli za historia ya familia, na nikajifunza kuhusu mababu zangu. Mama alisema wote wanawake na wanaume katika familia walikuwa na nywele ndefu sana, kama vile mimi. Kisha alisema kitu kimoja muhimu sana: mababu zangu wananisubiri katika ulimwengu wa kiroho! Alisema kwamba wanasubiri kubatizwa—kama vile ilivyonibidi kusubiri mpaka nilipokuwa na umri wa miaka minane ili kubatizwa. (Licha ya hayo, nilibatizwa katika kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa kwangu! Safi, siyo?)

Hivi ndivyo Hekalu la Bengaluru India litakavyoonekana wakati litakapokwisha kujengwa.

Picha
Friend, November 2021 Tier 2

Vielelezo na Patricia Castelao

Chapisha