2021
Msingi Wetu Imara
Novemba/Desemba 2021


Ujumbe wa Mkutano Mkuu kutoka kwa Nabii

Msingi Wetu Imara

Iliyotoholewa kutoka “Hekalu na Msingi Wako wa Kiroho,” Liahona, Nov. 2021.

Picha
President Nelson looking at Salt Lake Temple foundation

Hekalu la Salt Lake lilijengwa zaidi ya miaka 100 iliyopita. Waasisi walilijenga na vifaa vya wakati ule. Ni zuri sana. Lakini kama tutatazama msingi kwa karibu, tunaweza kuona kwamba baadhi ya mawe yamechakaa baada ya muda mrefu. Tunaweza pia kuona nyufa kati ya mawe na baadhi ya mawe yasiyo imara.

Wahandisi, wasanifu, na wajenzi sasa wanafanya kazi kuufanya msingi wa hekalu imara zaidi. Watakapomaliza, hekalu litakuwa imara vya kutosha kustahimili matetemeko ya ardhi na upepo mkali. Litakuwa imara vya kutosha kudumu kwa miaka mingi.

Lazima tujenge msingi wa maisha yetu juu ya mwamba wa Mkombozi wetu, Yesu Kristo. Kisha, wakati matetemeko ya ardhi ya kiroho yanapotokea, tutaweza kusimama imara.

Kila kitu tunachojifunza hekaluni kinatusaidia kuelewa zaidi kuhusu Yesu Kristo. Wakati msingi wako wa kiroho unapojengwa kwa uimara juu ya Yesu Kristo, hauhitaji kuogopa. Utaimarishwa na nguvu Yake.

Yesu Kristo ni Msingi Wangu wa Uhakika

Picha
coloring page of two children looking at statue of Jesus

Kushoto: Kielelezo cha Hekalu na Bailey Rees; picha ya Rais Nelson kwa hisani ya Habari za Kanisa; Kulia: Kielelezo na Bryan Beach

Chapisha