2021
Safari Yangu ya Kwanza Hekaluni
Novemba/Desemba 2021


Safari Yangu ya Kwanza Hekaluni

Picha
girl in dress, waving

Habari! Mimi ni Elena. Ni mara yangu ya kwanza kwenda hekaluni.

Picha
girl talking with bishop

Wiki chache zilizopita, nilikutana na askofu wangu. Aliniuliza maswali kadhaa kusaidia kuhakikisha kwamba nilikuwa tayari kwenda hekaluni. (Unaweza kusoma maswali kwenye ukurasa wa 22!) Kisha alinipa kibali changu mwenyewe cha hekaluni.

Picha
girl packing bag for temple, brother tying tie

Tunajitayarisha kwenda. Ninavaa mavazi yangu bora ya Jumapili. Mimi pia hupakia vitu kadhaa vya kurekebisha nywele zangu baada ya kuwa nimeloana. Na ninahakikisha ninacho kibali changu. Sasa tunaondoka kwenda kupanda basi!

Picha
girl and brother riding bus to temple in Spain

Lile pale ni hekalu! Ni zuri sana.

Picha
girl showing recommend at temple

Wakati ninapotembea ndani ya hekalu, ninajisikia amani. Ninaonesha kibali changu kwa mfanyakazi mwema wa hekaluni kwenye meza ya mapokezi. Mfanyakazi mwingine ananipa mavazi meupe. Ninakwenda kwenye chumba cha kabati dogo la kuwekea nguo ili kubadili nguo.

Picha
girl in white, standing by baptismal font

Sasa ninangojea zamu yangu ya kubatizwa. Wakati wa zamu ya kaka yangu, ninasimama karibu na kisima cha ubatizo kuwa shahidi. Ninahakikisha anazama kabisa ndani ya maji.

Picha
girl in white being baptized

Sasa ni zamu yangu! Maji ni ya uvuguvugu. Ninabatizwa kwa ajili ya watu kadhaa walio kwenye orodha.

Picha
girl being confirmed

Wakati ninapotoka majini, mfanyakazi wa hekaluni ananipa taulo. Ninajikausha katika chumba cha kubadilisha nguo na kurudia nguo zangu za Jumapili. Wakati ninapotoka, mfanyakazi wa hekaluni ananichukua ili kuthibitishwa kwa ajili ya watu kadhaa.

Picha
brother and sister leaving temple

Muda wangu hekaluni kwa kweli ulikuwa wa namna ya kipekee! Ninafurahi kwamba niliweza kusaidia wengine kwa kubatizwa na kuthibitishwa kwa ajili yao. Siwezi kungoja kurudi tena hivi karibuni.

Picha
Friend, November 2021 Tier 2

Vielelezo na Rachel Hoffman‑Bayles

Chapisha