2021
Kupata Kibali cha Hekaluni
Novemba/Desemba 2021


Kupata Kibali cha Hekaluni

Picha
picture of a temple recommend

Unapopata kibali chako cha hekaluni, utakuwa na usahili na askofu wako au rais wa tawi. Unaweza kumuuliza chochote unachotaka. Unaweza pia kuja na mzazi pamoja nawe, kama utapenda. Hapa ni baadhi ya vitu atakavyovizungumzia pamoja nawe.

Maswali ya Kibali cha Hekaluni

  • Je, una imani katika Baba wa Mbinguni, Yesu Kristo na Roho Mtakatifu?

  • Je, una ushuhuda wa Upatanisho wa Yesu Kristo na Urejesho wa Kanisa lake?

  • Je, unawakubali (kuwasaidia) Viongozi wako wa Kanisa (kama nabii, mitume, na askofu wako)?

  • Je, unajitahidi (kwa bidii) kuweka akili yako na mwili safi na pasipo waa?

  • Je, unafuata mafundisho ya Kanisa la Yesu Kristo kwa jinsi unavyowatendea wengine?

  • Je, unajitahidi kuishika kitakatifu Sabato?

  • Je, unajitahidi kuwa mwaminifu?

  • Je, unalipa zaka asilimia 10 kamili?

  • Je, unaelewa na kutii Neno la Hekima?

  • Kuna dhambi zozote nzito unahitaji kuzitubu?

  • Je, unahisi unastahili kuingia nyumba ya Bwana?

Picha
Friend, November 2021 Tier 2

Vielelezo na Emily Davis

Chapisha