2022
Kabla Hatujaja Duniani.
Januari/Februari 2022


Hadithi za Maandiko

Kabla Hatujaja Duniani.

Unaweza kusoma hadithi hii katika Ibrahimu 3:22–27.

Picha
Heavenly Father and Jesus

Kabla hatujazaliwa, tuliishi mbinguni pamoja na Baba yetu wa Mbinguni. Alitufundisha kuhusu mpango Wake wa furaha.

Picha
boy looking sadly at girl holding soccer ball

Baba wa Mbinguni alisema tungelikuja duniani ili kupata miili. Tungelijifunza na kufanya chaguzi. Nyakati zingine tungelifanya makosa. Tungemhitaji Mwokozi.

Picha
girl holding out soccer ball to boy

Mwokozi angetuonyesha jinsi ya kuishi. Na tunapokuwa tumefanya uchaguzi usio sahihi, tuweze kutubu.

Picha
Jesus standing with arms outstretched in front of earth

Yesu alisema, “Niko hapa, nitume mimi.” Baba wa Mbinguni alimchagua Yeye kuwa Mwokozi wetu. Yesu aliahidi kuja duniani ili kutuokoa sisi.

Picha
Jesus and Heavenly Father standing in beautiful garden

Ninaweza kumfuata Yesu. Siku moja nitaweza kurudi na kuishi pamoja na Baba wa Mbinguni.

Vielelezo na Apryl Stott

Chapisha