2022
Nitang’ara
Januari/Februari 2022


Ninaweza Kupiga muziki

Nitang’ara

Kwa kutafakari [robo noti] = 96–104

Picha
sheet music

1. Kuna Nuru ndani mwangu—

Nuru kamili ya Kristo—

Nimefanya ahadi.

Ya kuendelea kung’ara

Kwa kutembea katika hatua zake.

Na kufuata mpango Wake

Wakati wote na mahali po pote.,

Katika njia yo yote niwezayo

2. Tendo moja tu la ukarimu

Litainua nafsi iliyo pweke!

Neno moja la upole litalosemwa

Hugeuza huzuni kuwa tumaini.

Chaguo moja kama Yesu;

Litasambaza upendo aliotoa.

Na mmoja mmoja ulimwengu unakuwa

Mahali pazuri kuishi.

Kiitikio: Ninaangaza kama mshumaa gizani;

Ni cheche tu yahitajika kuleta tofauti.

Na ni rahisi kuona uangavu utaokuwa

Niachapo nuru yake ing’are kupitia mimi.

Niachapo nuru yake ing’are kupitia mimi.

Chapisha