Nyimbo na Mapovu ya Sabuni
Alice alichekacheka alipofikiria kuhusu Rais Kimball akiimba pamoja na ng’ombe.
Alice aliweka upawa wa tambi katika bakuli la kaka yake. Aliwapenda kaka zake na dada zake wadogo—wote watano! Alijisikia vizuri kuwasaidia. Lakini ilikuwa vigumu kuwa mkubwa nyakati zingine. Tangu mtoto mchanga alifike nyumba, amekuwa akisaidia zaidi. Mengi yamekuwa yakitendeka nyumbani kwao!
“Ulijifunza kuhusu nini Kanisani leo?” Baba aliuliza.
“Yesu!” Dada mdogo wa Alice alisema. Akapaka sosi ya tufaa kwenye sahani yake yote.
Alice alitabasamu. Sara alikuwa mrembo sana. Na mwenye uchafuzi pia.
“Nilijifunza kuhusu Rais Kimball …” Alice alianza kusema. Lakini mara Mama akaita kutoka chumba kingine. Alihitaji msaada wa Baba juu ya mtoto.
“Samahani,” Baba alisema. “Nitarudi sasa hivi.”
Wakati Baba anamsaidia Mama, Alice aliwasaidia wengine wote. Eric aliigonga glasi yake ya maziwa. Alice akasafisha. Sara alianza kulia. Alice akampa kumbatio. Clara alitaka kuongezewa tambi nyingine. Alice alimpa kiasi.
Hata Baba aliporudi, jikoni kulikuwa bado kuna kelele na kumechafuka. Alice alitamani kungelikuwa rahisi kujisikia amani.
Hatimaye, mlo wa mchana ulimalizika. Alice aliwasaidia nduguze kupeleka vyombo vyao kwenye sinki. Alice alikuwa mkubwa wa kutosha kutovunja vitu. Kwa hiyo yeye alikuwa kinara wa uoshaji wa vyombo. Alijaza sinki kwa maji yenye sabuni.
Natamani nisingekuwa nafanya kazi za nyumbani, Alice aliwaza. Kisha akakumbuka kile alichojifunza katika darasa la Msingi kuhusu Rais Spencer W. Kimball. Alipokuwa mdogo, naye alifanya kazi za nyumbani pia. Alizoea kuimba nyimbo za dini wakati akiwakamua ng’ombe maziwa.
Alice alipiga taswira ya Rais Kimball akiimba kwa sauti mbili na ng’ombe. Alichekacheka.
Kisha akapata wazo. Angeweza kuwa kama nabii! Akachukua kitabu cha nyimbo na akafungua wimbo wa kwanza.
Kwa kiasi fulani kilihitajika kiwekwe wazi. Hivyo Alice akakiweka dirishani. Akazuia upande mmoja wa kitabu na chungu cha maua. Kisha upande mwingine akazuia na kikombe kizito. Sasa aliweza kukiona wakati akifanya kazi zake.
Wakati Alice akisugua bakuli, vikombe, na vijiko, aliimba wimbo huo. Uvuguvugu wa mapovu ya sabuni, yalimfanya ajisikie vizuri mikononi. Na wimbo ulifanya moyo wake uwe na furaha.
Siku iliyofuata, Alice aliimba tena. Na hata siku baada ya siku. Alijaribu kukumbuka maneno ya kila wimbo. Halafu akauendea wimbo unaofuata. Alice alijifunza nyimbo nyingine pia! Alichukua mafunzo ya kupiga kinanda kwa miaka michache. Alipokuwa haujui wimbo, alijifunza noti zake kwenye kinanda.
Punde Alice hakuona taabu tena kuosha vyombo. Nyakati zingine ni kama alipenda kufanya hivyo! Ilikuwa vizuri kuimba na kufikiria kuhusu Yesu. Kujifunza kila wimbo mpya ilikuwa ni kama kupata rafiki mpya. Bila kujali maisha yalikuwa ya kelele kiasi gani, nyimbo za dini zilimsaidia kuhisi amani.